Thursday, June 18, 2015

ZIARA YA KINANA MKOANI GEITA, YATIKISA WILAYANI MBOGWE

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Kata ya Masumbwe, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Juni 17, 2015.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika katika kata ya Masumbwe, wilayani Mbogwe mkoani Geita.
 Katibu w NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo, wakati wa mkutano huo
 Mkuu wa wilaya ya Mbogwe akisalimia wananchi
 Wananchi wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Abdlrahman Kinana alipohutubia maelfu ya watu katika mkutano wa hadhara uliofanya katik kata ya Masumbwe,  utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati ya Kata ya Kashelo,  utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Wananchi wa Kata ya Kshelo, wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, baada ya kukagua na kushiriki ujenzi wa zahanati yao,  utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwapokea wanachama wapya wa CCM, waliohama kutoka Chadema, katika mkutano wa hadhara aliofanya katika Kijiji cha Lugunga,  utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na kijanaAugustine Gerald na kuahidi kumpeleka Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), alipokagua ujenzi wa nyumba ya Mwalimu katika Kijiji cha Lugunga,  utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimsikiliza kwa makini, Diwani wa Nyakafulwa, Mathias Nyororo, aliyekuwa akifafanua kutoanza kwa mradi wa maji kijiji cha Masumwe, licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa fedha za mradi huo miezi sita iliyopita. Iikuwa ni baada ya wananchi kulalamika kutopata maji katika kijiji hicho katika mkutano wa hadhara ambao Kinana aliufanya katika kata ya Masumbwe,  utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivuka kwenye daraja duni, wakati akienda kukagua mradi wa ujenzi wa shule katika kijiji cha Lyamchele,  utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita, jana, Juni 16, 2015. Tayari serikali imeanza mpango wa ujenzi wa daraja imara katika Kijiji hicho. 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisafirishwa kwa pikipiki, baada ya kuvuka daraja duni kwenda kijiji cha Lyamchele kukagua ujenzi wa shule,  utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
 Wananchi wa Kijiji cha Lyamchele, wakiwasindikiza kwa ngoma na Kisukuma, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule katika kijiji hicho.
Vijana wanaojishughulisha na kutafuta madini ktika udongo wa masalia, wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO).
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.