Friday, June 5, 2015

KINANA AWASILI MKOANI KAGERA SALAMA KWA BASI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Ndugu Idd Ame wakati wa mapokezi katika mkoa wa Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM anahitimisha ziara katika mikoa wa Kagera ,Geita na Mwanza na kumfanya awe amezunguka mikoa na majimbo yote nchi nzima,ambapo Katika mikoa hii mitatu iliyobaki, atakagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM,kukiimarisha Chama cha Mapinduzi pamoja na kuhimimiza uandikishaji kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Costansia Buhiye mara baada ya kuwasili Nyakanazi mkoani Kagera ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake ya siku 10 katika mkoa wa Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbali mbali wa CCM mkoa wa Kagera waliokuja kumlaki.

 Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na wakazi wa Nyakanazi mkoani Kagera.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiwa amembeba  mtoto Aloyce Atukuzwe wakati wa kusalimia wananchi wa Nyakanazi mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia kikundi cha ngoma wakati wa mapokezi Nyakanazi mkoani Kagera.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa Nyakanazi waliojitokeza kwa wingi kwenye mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM na msafara wake mkoani Kagera.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Costansia Buhiye akisalimia wananchi wa Nyakanazi na kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkoa wa Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyakanazi waliojitokeza kumpokea ambapo anategemewa kuwa na ziara ya siku 10 mkoani Kagera.
(Picha zote na Adam Mzee)

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.