Friday, June 12, 2015

KINANA ATINGA JIMBO LA KYERWA LEO, ATAKA MIRADI YA MAENDELEO ISIMAMIWE NA HALMASHAURI BADALA YA SERIKALI

Wananchi wakimsalimia kwa shauku, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, alipowasili Uwanja wa michezo, kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibingo, Kata ya Kaisho, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, leo.
Katibu wa EC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwapungia mkono, wananchi waliofurika kwenye Viwanja vya michezo, katika Kijiji cha Kibingo, Kata ya Kaisho, baada ya kuwasili na Kinana kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika eneo hilo leo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibingo, Kata ya Kaisho, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenzi Nap Nnaauye akizungumza kabla ya Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, kukaribishwa jukwaani, kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibingo, Kata ya Kaisho, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, leo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimsaidia kunyanyua ndoo, Asha Katanga, aliyefika kuchota maji baada ya Katibu Mkuu huyo, kuzindua rasmi mradi wa maji wa Kijiji cha Kibingo, wilayani Kyerwa,  akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, leo. Mama huyo ana mototo mchanga ambaye amejifungua hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo,Odeta Elieza, aliyefika kuchota maji baada ya Katibu Mkuu huyo, kuzindua rasmi mradi wa maji wa Kijiji cha Kibingo, wilayani Kyerwa,  akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, leo.
Mkulima bora wa migomba na kahawa katika Kijiji cha Mabira, Kishunge Ntibalienda (kulia) akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuhusu alivyoweza kufanikiwa katika kilimo cha mazao hayo, Katibu Mkuu alipomtembelea mkulima huyo,  akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, leo.
Mkulima bora wa migomba na kahawa katika Kijiji cha Mabira, Kishunge Ntibalienda (kulia) akimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuhusu zao la kahawa linavyostawi, Katibu Mkuu alipomtembelea mkulima huyo,  akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wananchi katika mkutano wa Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana aliofanyika leo katika Kijiji cha Mabira, wilayani Kyerwa mkoani Kagera leo.
Wananchi wa Kijiji cha Mabira wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mabira leo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera.
Katibu wa NEC, itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia Nesi Mkuu, yeye na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, walipowasili kwenye zahanati ya Kigorogoro, wilayani Kyerwa mkoani Kagera leo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye zahanati ya Kigorogoro, wilayani Kyerwa mkoani Kagera leo
Kinana akiendelea kukagua Zahanati hiyo
Wananchi wa Kijiji cha Kigorogoro katika Kata ya Murongo wilayani Kyerwa mkoani Kagera wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCm, Abdulrahman Kinana akipowasili kuwahutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutuia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kigorogoro, kata ya Murongo wilayani Kyerwa mkoani Kagera leo.
Mpaka wa Tanzania na Uganda wa mto Kagera, katika kijiji cha Isingiro, wilayani Kyerwa mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili katika Kijiji cha Mulongo, wilayani Kyerwa mkoani Kagera kukagua ujezi wa soko la Kisasa katika kijiji hicho leo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika kijiji hicho leo.
Wanakijiji cha Murongo wakimshangilia kwa bashasha Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Miongo, alipowasili katika kijiji hicho kukagua ujenzi wa soko la kisasa katika kijiji hicho leo. hata hivyo Kinana ameonyeshwa kusikishwa baada ya kujulishwa kuwa ujenzi wa mradi huo, unaohitaji sh. bilioni 1.5 umesimama kutokana na serikali kuu kukosa fedha. 
        Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, amesema ni vema miradi uhimu ya maendeleo maendeleo iwekwe chini ya usimamizi wa halmashauri ya eneo linalohusika badala ya serikali kuu. 
       Amesema, utaratibu wa kuifanya miradi ya aina hiyo kuwa chini ya usimamizi wa serikali, umekuwa ukileta matokeo mabaya ikiwemo kusimama kwa ujenzi wa miradi.
       Kinana amesema hayo leo, baada ya kukagua ujenzi wa kitu kikubwa cha biashara, katika Kata ya... wilayani Kerwa mkoa ni Kagera ambacho ujenzi wake umesimama tangu mwaka juzi kwa maelezo ya kukosekana fedha.
      "Jamani jengo kama hili lilitakiwa lisimamiwe na Halmashauri ya eneo hili, lakini kusimamiwa na wizara ni kupoteza muda, hivi kweli ni rahisi mkaguzi atoke Dar es Salaam, kuja hadi huku kukagua ujenzi tu wa jengo hili, hasa ikizingatiwa kuwa miradi kama hii ni mingi?" alihoji Kinana.

Katibu kuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela baada ya Kinana kukagua ujezi wa soko la Kisasa katika Kijiji cha Mulongo, Wilayani Kyerwa mkoani Kagera leo
Kabla ya kuanza ziara yake katika wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alianza kazi kwa kuzungumza na wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCm ya wilaya hiyo (Pichani), leo asubuhi. Picha na CCM Blog
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.