Monday, June 22, 2015

KINANA AMALIZA ZIARA JIMBO LA SENGEREMA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa watu waliofurika kumsikiliza katika uwanja wa CCM Wilaya ya Sengerema ambapo aliwaambia wakazi hao Chama Cha Mapinduzi kitasimamia haki na misingi kwani ndio chama pekee kinachojali watu.

Umati wa wakazi wa Sengerema wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia kwenye viwana vya CCM wilaya.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Sengerema mjini kwenye uwanja wa CCM wilaya ambapo aliwaambia moja ya sababu kubwa ya kuporomoka kwa vyama vya upinzani nchini ni kutotaka kubadili viongozi na kubaki na viongozi wale wale ambao tangia 1995 mpaka leo wameshindwa kuleta mabadiliko kwenye vyama vyao na kuendelea kushindwa kwenye chaguzi.
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.Magessa Mulongo akihutubia wakazi wa Sengerema ambapo alizungumzia namna ya zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye daftari la kudumu linaoendelea vizuri mkoani hapo .
 Mbunge wa Jimbo la Sengerema Ndugu William Ngeleja akihutubia wakazi wa Sengerema mjini kwenye mkutano wa hadhara amabao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni rasmi.
 Wananchi wakisikiliza hotuba za viongozi wao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maendeleo ya ujenzi wa tanki la maji kwenye vilima vya Igogo, Sengerema mkoani Mwanza.
 Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mhe.William Ngeleja akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa kuona maendeleo ya ujenzi wa tanki kubwa la maji Igogo,Sengerema.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata mpya ya Nyamizeze, Sengerema ambao walitaka kumsalimia .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Nyamazugo kutoka kwa Mhandisi wa Maji mkoa wa Mwanza Ndugu Antony Sanga.
Mradi huo mpaka kukamilika utakuwa na uwezo wa kutoa lita milioni 15 hivyo kuzidi mahitaji ya Sengerema ambayo ni lita milioni 8 kwa sasa,awamu ya kwanza ya mradi huo unategemewa kukamilika mwezi wa 8 mwaka huu na awamu nyingine inategemewa kukamilika mapema mwaka 2016.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maendeleo ya ujenzi wa miundo mbinu ya maji katika chanzo cha maji kilichopo katika kijiji cha Nyamazugo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi kabla ya kuzindua kivuko kipya cha SUMAR III, Kamanga, wilaya ya Sengerema.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa kivuko kipya cha SUMAR III kitakachokuwa kinatoa huduma kati ya Sengerema na Mwanza.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaini kitbu cha wageni baada ya kuzindua kivuko kipya cha SUMAR III.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Sengerema Ndugu William Ngeleja pamoja na mmiliki wa kivuko cha SAMAR III Ndugu Salum Ally (kulia) mara baada ya uzinduzi wa kivuko hicho kukamilika.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.