Friday, June 5, 2015

KINANA AKUTANA NA WAFUGAJI NYAKANAZI

  • Asikitishwa na kutopatikana kwa ufumbuzi wa mgogoro kati ya wafugaji na hifadhi
  • Wafugaji wamwambia Kinana wamekaa vikao 17 na viongozi wakubwa wa kitaifa lakini hakuna utatuzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya mkoa w
 Mwenyekiti wa chama wa Wafugaji Kanda ya Ziwa Ndugu Juvinale Murashani akizungumza kwenye kikao cha wafugaji na Katibu Mkuu ambapo alimuelezea matatizo mbali mbali yanayowakabili wafugaji hasa mgogoro wao na hifadhi ya Kimisi.
 Mkuu wa Wilaya ya Ngara Ndugu Costantine Kanyasu akielezea namna anavyouelewa mgogoro wa wafugaji na ushari alioutoa kwa watu wa hifadhi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wafugaji kwenye kikao kilichofanyika Nyakanazi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchama wa chama cha wafugaji kanda ya ziwa waliojitokeza kwa wingi kueleza mgogoro wao na hifadhi ya Kimisi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa kupelekwa eneo ambalo limekuwa na uharibifu sana wa mazingira pamoja na mifugo inayokamatwa kuwekwa hapo.

 Wafugaji wakimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana sehemu ambayo mifugo huzuiwa baada ya kukamatwa na watu wa hifadhi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteremka kwa kukimbia kwenye kilima ambacho mifugo huzuiwa na watu wa hifadhi
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa Chamilwa njia panda ya Chato ambao walijitokeza kumsalimu Katibu Mkuu na msafara wake ambao wamewasili na basi kutokea Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa Chamilwa njia panda ya Chato waliojitokeza kumsalimu.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Ndugu John Mongella akiwasalimia wananchi wa Chamilwa njia panda ya Chato ambao walijitokeza kumsalimu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye ameanza ziara ya siku 10 mkoani Kagera.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na mbunge wa Bukoba mjini Balozi Hamisi Kagasheki mara baada ya kuwasili Bukoba mjini tayari kwa ziara za kujenga na kuimarisha chama.

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.