Saturday, June 6, 2015

KINANA AWAPA POLE FAMILIA YA MAREHEMU MZEE SAMUEL LUANGISA BUKOBA LEO

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha maombolezo ya Mzee Samuel Luangisa aliyefariki  Jumatatu Mei 25,2015 saa tano asubuhi jijini New York.

 Mzee Samuel N. Luangisa ni mzaliwa wa Bukoba na mmoja kati ya waasisi wa TANU na hatimaye CCM, ambaye alipata kuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa baada ya uhuru (1961–1964).
Mzee Luangisa ni miongoni mwa watu waliopendekeza jina la Mkoa wa Kagera badala ya jina la awali la Mkoa wa Ziwa Magaharibi.
Jina hilo lilibadilishwa na kuwa “Kagera” mwaka 1979, mara baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda, ambapo mkoa, chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa, aliyekuwepo wakati huo, Capt. Peter Kafanabo, ulipendekeza uitwe “Kagera”chini ya ushauriano wa Mzee Luangisa.
Luangisa alipata kuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM kwa muda mrefu, na baada ya hapo ameendelea kuwa Diwani wa Kata ya Kitendaguro anakozaliwa hadi 2014

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha maombolezo ya Mzee Samuel Luangisa
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mzee Samuel Luangisa.
 Kinana akitoa heshima katika kaburi la Mzee Samuel Luangisa
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pole mke wa marehemu Samuel Luangisa.Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.