Tuesday, June 23, 2015

KINANA AANZA ZIARA JIMBO LA MISUNGWI ASUBUHI HII, NI BAADA YA KUPANDA KIVUKO KUTOKA SENGEREMA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakipanda Kivuko cha Mv Misungwi, kutoka Feri ya Kigongo wilayani Sengerema kwenda Kivuko cha Usagara kwenda  jimbo la Misungwi kuendelea na ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika mkoa wa Mwanza, leo.
 Katibu kuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akionyeshana miamba ya mawe katika ziwa Vicoria wakati wakiwa kwenye kivuko mv Misungwi, wakati wakienda jimbo la Misungwi leo. Kushoto ni Katbu wa CCM mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu.
 Miamba ya mawe yaliyopangana kwa aina yake katika ziwa Victoria ambayo Kinana na Ngeleja walikuwa wakionyeshana.
 Baadhi ya maofisa wa CCM wakiwa kwenye Kivuko wakati wa safari hiyo kwenda Misungwi
 Baadhi ya madereva waliopo kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakiwa kwenye kivuko hicho
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasili Feri ya Usagara baada ya kufika eneo hilo kwa Kivuko cha Mv Misungwi. Pamoja naye ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimia baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Miisungwi waliofika kumlaki kwenye Feri ya Usagara leo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimia na Mbunge wa zamani wa jimbo la Misungwi ambaye sasa ni Mjumbe wa NEC, Jacob Shibiriti wakati wa mapokezi hayo kwenye Feri ya Usagara.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimshauri jambo, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, walipokuwa katika mapokezi hayo kwenye Feri ya Usagara
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitazama ngoma wakati wa mapokezi yake kwenye Feri ya Usagara baada ya kuwasili kwa kivuko.
 Mapokezi hayo kwenye Feri ya Usagara
 Mkurugenzi wa Wilaya ya Misungwi, Nathan Mshana akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, alipofika kukagua ujenzi wa Zahanati katika kijiji cha Nyang'honyango, katika wilaya hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza baada ya kupewa taarifa ya mradi huo wa ujenzi wa Zahanati. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo na Katibu wa CCM mkoa huo, Miraji Mtaturu.
 Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akishriki kupachika dirisha kwenye zahanati hiyo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu kwenye zahanati hiyo
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akipanda mti wa kumbukumbu kwenye Zahanati hiyo.
 Mbunge wa MisungwiCharls Kitwanga akipanda mti wa kumbukumbu kwenye Zahanati hiyo
 Wanakwaya wakiiba kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili kuzindua Ofisi ya CCM Kata ya Nyang'honyanga, wilayani Misungwi mkoani Mwanza leo
Kinana akizungumza baada ya kupewa taarifa ya ujenzi wa Ofsi hiyo ya CCM
 Kinana akikabidhi kadi kwa mwanachama mpya wa CCM kwenye ofisi hiyo ya CCM
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipandisha bendera kuashiria uzinduzi wa Ofisi hiyo. Picha zote na Bashir Nkoromo na Adam Mzee, CCM Blog
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.