Saturday, May 9, 2015

WAPINZANI WAJIUZULU UINGEREZA BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZIKiongozi wa chama cha Leba nchini Uingereza Ed Miliband amewaambia wanaharakati wa chama hicho kwamba anajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho kufuatia matokeo duni ya uchaguzi mkuu.
Miliband ambaye amempongeza Waziri mkuu David Cameron kwa kuchaguliwa kwa awamu ya pili amesema kuwa anachukua jukumu la kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi huo.
Chama cha leba kilishindwa vibaya katika uchaguzi huo.
Katika hotuba aliyotoa mjini London,Miliband alisema kuwa ni wakati mtu mwengine anafaa kuchukua uongozi wa chama hicho huku akithibitisha kuwa naibu kiongozi wa chama hicho Harriet Harman atashikilia uongozi kwa muda.

Bwana Miliband alipongezwa na wafanyikazi wengine alipowasili katika makao makuu ya chama cha leba katikati mwa London

Wakati huohuo Nick Clegg amejiuzulu kama kiongozi wa chama cha Liberal Democrat kufuatia matokeo yalioonyesha kuwa chama cha Conservative kinaelekea kushinda uchaguzi huo.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.