LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 12, 2015

VIONGOZI WASHIRIKI KWA WINGI KUTOA HESHIMA YA MWISHO KWA JOHN NERERE


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu John  
Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. Marehemu John 
anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa 
marehemu John Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. 
Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya viongozi na waombolezaji nyumbani kwa Mama Maria 
Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu John Nyerere. Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani 
kwao Butiama. Picha na OMR
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk.Wilbroad Slaa wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu John Nyerere.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mama Salma Kikwete akisaini kitabu cha rambi rambi kwenye msiba wa John Nyerere
 Makama Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba kwenye msiba wa John Nyerere .

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa kwenye msiba wa John Nyerere ambapo viongozi mbali mbali walijumuika kutoa heshima za mwisho.

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akimuonyesha jambo Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)Philip Mangula kwenye msiba wa John Nyerere ,msasani jijini Dar es salaam.(Picha na Adam Mzee)
 Makongoro Nyerere akisoma wasifu wa Marehemu John Nyerere
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa heshima ya mwisho kwa mwili wa marehemu John Nyerere.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages