Tuesday, May 5, 2015

RAIS KIKWETE AMREJESHA NYUMBANI BALOZI LIBERATA MULAMULA, AMTEUA KUWA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Rais Jakaya Kikwete amemteua Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Balozi Liberata Rutageruka Mulamula (Pichani), kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Pia Rais Kikwete amemteua Mkurugebzi waIdara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Hassan Simba Yahya kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema uteuzi huo umeanza jana.

Taarifa hiyo imesema, Rais amemteua Mzee Pius Msekwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, huku akimteua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi mkoa wa Tanga,  Daudi Maayeji kuwa Mkurugenzi wa Jiji la mkoa huo wa Tanga.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.