Sunday, May 10, 2015

NAPE AWATAKA VIJANA KUWEKA ITIKADI PEMBENI KWANZA NA KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akishiriki mazoezi ya kukimbia mchaka mchaka yalioandaliwa na kikundi cha Tegeta Jogging and Sports Club .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye pamoja na viongozi wengine na makada wa CCM wakishiriki mazoezi ya kukimbia mchaka mchaka yalioandaliwa na kikundi cha Tegeta Jogging and Sports Clubikiwa sehemu ya uzinduzi wa klabu hiyo ya michezo na mazoezi ya Tegeta.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akikatiza mitaa ya Tegeta shule wakati wa kuhitimisha  mazoezi ya kukimbia mchaka mchaka yalioanzia Tegeta kwa ndevu kupita njia panda ya kiwanda cha saruji Wazo na kuhitimishwa kwenye viwanja vya Tegeta shule .
Kikundi cha Msasani Jogging kikishiriki mazoezi  ya viungo kwenye uwanja wa Tegeta shule wakati wa sherehe za uzindiz wa klabu ya michezo na mazoezi ya Tegeta Jogging and Sports Club ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kishiriki mazoezi ya viungo wakati wa uzinduzi wa klabu ya mazoezi na michezo Tegeta.
 Mazoezi ya viungo
 Watoto hawakuwa nyuma wakati wa kushiriki mazoezi.
 Kutoka kushoto ni Diwani wa Viti maalum Kinondoni Florence Wasira, Diwani mwingine wa Viti maalum Bernadette Ritti kutoka Kinondoni pamoja na kada wa CCM Gabriel Munasa wakiwa sehemu ya wageni walioshiriki katika kufanikisha uzinduzi wa kikundi cha Tegeta Jogging and Sports Club.
 Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es salaam Juma Simba Gadafi akiwasalimia vikundi vilivyoshiriki sherehe hizo za uzinduzi wa klabu ya michezo na mazoezi ya Tegeta.
 Katibu wa Kikundi cha Tegeta Jogging and Sports Club Mariam Said akisoma risala mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nauye wakati wa sherehe wa uzinduzi wa kikundi chao.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikundi cha michezo cha Tegeta Jogging and sports club ambapo aliwaambia vijana wajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura kwanza na kuweka itikadi za vyama pembeni, pia alitoa pongezi kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi William Lukuvi kwa kazi nzuri ya kusimamia viwanja vya wazi vilivyovamiwa hasa katika wilaya ya kindondoni virudi visaidie katika kukuza michezo.
Kada wa CCM Gabriel Munasa akiwasalimia wana vikundi vya Jogging na kuahidi kuvisaidia katika kila hali katika kufanikisha malengo yao.
 Mariam Said akihamasika wakati wa mazoezi kwenye uwanja wa shule Tegeta.
 Watoto Mohamed Said nwenye umri wa miaka 14 (kushoto) Mbwana Sharifu mwenye umri wa miaka 13 kutoka Fanja Jogging wakipasha misuli kabla ya kuanza mchaka mchaka.
 Wadada wakiruka kamba kabla ya kuanza jogging
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipata kifungua kinywa baada ya kumaliza kushiriki jogging
(Picha zote na Adam Mzee)


Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.