Friday, May 22, 2015

JK AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM MJINI DODOMA

 Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akifungua kikao cha kawaida cha Kamati Kuu mjini Dodoma, wengine pichani ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia).
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma utangulizi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma.
 Katibu wa Itikadi na UeneziCCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akisoma jambo kwenye kompyuta yake muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao.
 Mjumbe wa Kamati Kuu Alhaji Adam Kimbisa akibadilishana mawazo na Mjumbe mwingine wa Kamati Kuu Mwigulu Lameck Nchemba kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma muda mchache kabla kikao hakijaanza.
Mjumbe wa Kamati Kuu Mhe.Pindi Chana akiteta jambo na Mjumbe mwingine wa Kamati Kuu Mhe. Jenista Mhagama pembeni ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Abdala Bulembo muda mchache kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.