LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 10, 2015

CCM ARUSHA YATOA ONYO KWA WALIOTANGAZA NIA ARUSHA MJINI

Moses Mashalla, Arusha
Chama Cha Mapinduzi(CCM)  wilayani Arusha kimetoa  onyo kwa wagombea waliojitokeza kutangaza nia ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupiti chama hicho kuacha tabia ya kuchafuana na kuanza kampeni kabla ya muda.

Onyo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na katibu wa chama hicho wilayani Arusha,Ferooz Bano wakati akimkabidhi kanuni za uchaguzi wa CCM mgombea alliyetia nia ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupitia chama hicho,Kim Fute .

Mgombea huyo alifika mbele ya ofisi za CCM wilayani hapa kujitambulisha  na kutia nia ambapo mbali na kufanyiwa ukaguzi wa kadi zake za uanachama pia alikabidhiwa kitabu chenye kanuni hizo na kupewa agizo la kutoshiriki kampeni kabla ya muda.

Hadi sasa jumla ya wagombea saba  ambao ni Kim Fute,Phillemon Mollel”Monaban”,Mustapha
Panju”Bushbuck”,Victor Njau,David Rwenyagira,Deo Mtui,Francis Laiser pamoja na mbunge mstaafu wa jimbo la Arusha mjini,Felix Mrema wamejitokeza kutia nia kuwania jimbo la Arusha mjini.

Akizungumza mara baada kumkabidhi kanuni hizo katibu huyo wa wilaya aliwataka wagombea wote waliojitokeza kutia nia kupitia chama hicho kuacha tabia chafu ya kupakana kuandaa sherehe kwa wapiga kura.

“Muda wa kampeni bado haujafika hatutaki  nyinyi wagombea muanze kuchafuana huko mitaani na wala kuandaa vijisherehe”alisema Bano

Hatahivyo,kwa upande wake mgombea huyo mbali na kushukuru mapokezi ofisini hapo pia alihaidi kufuata maagizo ya chama hicho na kusisitiz kwamba atafuata maagizo ya kanuni hizo kwa umakini mkubwa.

Fute, alitangaza rasmi kuinga katika kinyang”anyiro hicho kupitia CCM huku akijitapa kwamba amejipima na kubaini anatosha kuwa mwakilishi wa jimbo la Arusha mjini kwa kuwa amegundua kuna ombwe la uongozi.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages