LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 11, 2015

MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA MBEYA AVUTIWA NA VIPAJI VYA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI PANDAHIL


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) mkoani Mbeya Aman Kajuna Mwenye suti Nyeusi akiwa katika  mahafali ya kidini ya kasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Pandahill iliyopo wilayani hapa
Burudani ikitolewa kwa wanafunzi wa shule hiyo wakati wa  mahafali ya kidini ya kasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Pandahill iliyopo wilayani hapa
wahitimu







Burudani ikitolewa na baadhi ya wanafunzi katika   mahafali ya kidini ya kasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Pandahill iliyopo wilayani hapa


hapo sasa viduku kwenda mbele









Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) mkoani Mbeya Aman Kajuna akizungumza katika  kwenye mahafali ya kidini ya kasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Pandahill iliyopo wilayani hapa.




Maombi kwa wahitimu


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) mkoani Mbeya Aman Kajuna akigawa vyeti kwa hatimu wa mahafali ya kidini ya Ukwasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Pandahill iliyopo wilayani hapa.



Na Mwandishi wetu,Mbeya
WAHITIMU katika shule za sekondari nchini wameshauriwa kuviendeleza vipaji vya sanaa wanavyoonesha kwenye sherehe mbalimbali wakiwa shuleni wakitambua kuwa vina mchango mkubwa katika kuwapa ajira maishani mwao.



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) mkoani Mbeya Aman Kajuna alitoa ushauri huo kwenye mahafali ya kidini ya Ukwasifeta ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu katika shule ya sekondari ya Pandahill iliyopo wilayani hapa.



Kajuna alitoa ushauri huo baada ya kukunwa na vipaji mbalimbali vya sanaa walivyoonesha wahitimu na wanafunzi wanaobaki kama ilivyowafurahisha pia waalikwa wengine ukumbini hapo.



Miongoni mwa vipaji vilivyooneshwa na wanafunzi wa shule hiyo ni pamoja na uimbaji wa nyimbo za injili uliodhihirisha kwa kiasi kikubwa wanafunzi hao wanao uwezo mkubwa wa kutunga na kuimba tenzi na mashairi ya nyimbo mbalimbali.



Sanaa nyingine ni uchezaji wa aina mbalimbali wa nyimbo za injili,Uongozaji wa sherehe,uchekeshaji na upigaji wa vyombo vya muziki zikiwemo ngoma na kinanda.



Kajuna alisema si wakati tena kwa wanafunzi kuacha sanaa hizo zikaishia mashuleni,badala yake wahakikishe wanaziendeleza hata wafikapo katika vyuo na baadaye wazifanyie kazi katika kuwapa ajira badala ya kubaki wakitegemea kuajiriwa pekee.



“Kama mna vipaji kama mlivyoonesha hapa sidhani kama mnapaswa kuwa miongoni mwa watanzania ambao katika miaka kadhaa ijayo watatakiwa watembee kutwa nzima na bahasha za kaki wakipita kila ofisi kuomba kazi.Unatembea mchana kutwa mpaka bahasha inachanika upande wa juu.Uliiweka kiganjani baadae unaamua uiweke kwapani”



“Tumieni vipaji vya sanaa mliyoonesha hapa kujiajiri katika miaka hiyo.Huu ni utajiri tosha unaoweza kuwapa maisha bora tena pasipo kutumia gharama kubwa kama ilivyo kwa wengine.Mmeonesha mnaweza” alisisitiza mwenyekiti huyo wa uvccm mkoa.



Hata hivyo Kajuna alisema mchango wa wazazi,walezi na wadau wengie ndiyo msingi mkubwa katika kuendeleza vipaji vya sanaa walivyo navyo wanafunzi hivyo akawaasa kutambua vipaji wal;ivyonavyo watoto wao.


Mwisho

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages