Wednesday, April 15, 2015

MICHUANO YA SOKA JIMBO LA TEMEKE, MTEMVU CUP, YAANZA KUFUNGULIWA RASMI LEO

 Zawadi mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha Michuano ya Soka Jimbo la Temeke, Mtemvu Cup, vikiwa tayari wakati wa kukabidhi jezi, kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo, leo, kwenye viwanja vya Chuo Cha Bandari, Temeke jijini Dar es Salaam.
 Vijana wa hamasa wakishangilia wakati wa shamrashamra za uzinduzi wa michuano hiyo kenye Uwanja wa Chuo Cha Bandari, Dar es Salaam, leo
 Wasanii wa kikundi cha Machozi  cha jimboni humo, wakitumbuiza kwa ngoma wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo leo
 Mbunge wa jimbo la Temeke Abbas Mtemvu akivishwa nyoka na wasanii waliocheza ngoma ya majoka, wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo leo
  Mbunge wa jimbo la Temeke Abbas Mtemvu akivishwa nyoka na wasanii waliocheza ngoma ya majoka, wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo leo
 Msanii wa Kikundi cha Mapambano Theatre cha temeke, Helen John akionyesha uhodari wake wa kucheza hukuwa akiwa amejipamba kwa nyoka, wakati wa uiznduzi wa michuano hiyo.
 Msanii wa Kikundi cha Mapambano Theatre cha temeke, Helen John akionyesha uhodari wake wa kucheza hukuwa akiwa amejipamba kwa nyoka, wakati wa uiznduzi wa michuano hiyo.
 Mwenyekiti wa CCM, wilaya ya Kinondoni Salum Madenge (kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu (wapili kulia), wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo leo.Watatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke, Yahya Sikunjema.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Temeke, Yahaya Sikunjema (wa pili kulia), akimkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa CCM Kata ya Azimio, Essa Uswege kwa ajili ya mashindano ya Mtemvu Cup yaliyozinduliwa  jijini Dar es Salaam leo jioni. Kulia ni Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu aliyeanzisha mashindano hayo na kushoto ni Diwani wa Kata ya Azimio, Hamisi Mzuzuri. 
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke Yahya Sikunjema, akimkabidhi vifaa vya michzo, Diwani wa Kata ya Miburani, Juma Nkenga, wakati wa uzinduzi wa michuano ya soka jimbo la Temeke, Mtemvu Cup 2015, leo kwenye Viwanja vya Chuo Cha Bandari jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke Yahya Sikunjema, akimkabidhi vifaa vya michzo, Diwani wa Kata ya Kurasini, Wilfred Kimani, wakati wa uzinduzi wa michuano ya soka jimbo la Temeke, Mtemvu Cup 2015, leo kwenye Viwanja vya Chuo Cha Bandari jijini Dar es Salaam. Timu kutoka kata zote za jimbo hilo kila maja imepewa vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na jezi na mipira.
 Mke wa Mbunge wa Temeke, Mama Mtemvu (kushoto) akifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo
 Msanii anayetamba kwa jina la Msagasumu, akihamasisha vijana kwa nyimbo zake, wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo leo
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Memvu, Madenge na sikunjema wakifuatilia wakati timu za Vituma na Kata ya 14 zikipepetana kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo.
Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akiwasalimia wachezaji wa timy ya Yombo Vituka kabla ya kuanza kwa mashindano hayo dhidi ya timu Temeke Kata ya 14.
 Kipa wa timu ya Kata ya 14, Frank Ahmed akiokoa hatari golilini wakati mshambuliaji wa timu ya Yombo Vituka, Seif Ally alipotaka kupachika bao, wakati wa mechi ya fungua dimba ya Michuano ya Soka Jimbo la Temeke, Mtemvu Cup 2015, leo kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke Dar es Salaam. Katika mechi hiyo timu hizo zimetoshana nvugu kwa kufungana bao 1-1.
 Mchezaji wa timu ya Yombo Vituka Seif Ally (kushoto) akiumiliki mpira huku akiandamwa na mchezaji Charles Magige wa timu ya Kata ya 14, wakati wa mechi ya fungua dimba ya Michuano ya Soka Jimbo la Temeke, Mtemvu Cup 2015, leo kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke Dar es Salaam. Katika mechi hiyo timu hizo zimetoshana nvugu kwa kufungana bao 1-1.
Mchezaji wa Yombo Vituka Brighton Sapa (kushoto), akipambana na mchezaji wa  timu ya Kata ya 14, Rashid Kapate, wakati wa mechi ya fungua dimba ya Michuano ya Soka Jimbo la Temeke, Mtemvu Cup 2015, leo kwenye Uwanja wa Mwembe Yanga, Temeke Dar es Salaam. Katika mechi hiyo timu hizo zimetoshana nvugu kwa kufungana bao 1-1. Picha zote na Bashir Nkoromo- theNkoromo Blog
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.