Sunday, March 15, 2015

ZIARA YA KINANA NGORONGORO YAIBUA MENGI

  • Wananchi wamuelezea matatizo yao ya ardhi ,maji,barabara na mawasiliano ya simu
  • Aahidi kuwakutanisha wananchi na Waziri wa Ardhi na Waziri wa Maliasili
  • Awapongeza wananchi hao kwa umoja na mshikamano wao

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wanakijiji cha Ngaresero kilichopo kata ya Loliondo

Zakayo Sironga Oloidimaye mkazi wa kata ya Ngaresero ,Ngorongoro ,akiuliza swali linaluhusu mipango ya kuwaletea hudumaza mtandao ili waweze kupiga simu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa mapokezi uliofanyika Ngarasaoo ikiwa sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM kupita jimbo kwa jimbo , wilaya kwa wilaya nchini lengo likiwa kuimarisha Chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
 Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Ngaresero kilichopo Loliondo wilaya ya Ngorongoro.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Elias Ngorisa ambaye pia ni diwani ya kata ya Malambo akizungumzia mipango ya halmashauri kusaidia kushuriki ujenzi wa madara katika shule ya sekondari Samunge
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Samunge kabla ya kushiriki ujenzi wa shule ya sekondari Samunge wilayani Ngorongoro
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi  wa madarasa ya kidato cha tano na cha sita katika shule ya sekondari ya Samunge kulia ni Mbunge wa Ngorongoro, Saning'o Ole Telele
 Watoto wa kimasai wa kijiji cha Mdito wakiwa juu ya kichuguu wakiangalia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM (haupo pichani)ukipita kijijini kwao .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Loliondo Sakala.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa tank la maji katika kijiji cha Loliondo Sakala.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Wasso Ndugu Revocatus William Parapara.
Awali ndugu Revocatus Willim Parapara alikuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Ngorongoro kwa takribani miaka 15.
 Wananchi wa Kata ya Wasso wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Wasso wilaya ya Ngorongoro.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Wasso wilaya ya Ngorongoro ambapo aliwaambia viongozi wa wananchi wa wilaya hiyo lazima waifanyie kazi migogoro ya ardhi na mgawanyo wa madaraka kwa mapana zaidi ili kulinda umoja na mshikamano wa wananchi na kuhakikisha haki zinatendeka kwa kila mtu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi ya Chadema baada ya kuipokea kutoka kwa aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA wilaya ya Ngorongoro ,Bi.Elinami Limbali ambaye amejiunga na CCM yeye pamoja na viongozi wengine wanne.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.