Thursday, March 5, 2015

ZIARA YA KINANA JIMBO LA KIBAKWE YAWAFURAHISHA WANANCHI

  • Wengi wavutiwa na hotuba zake
  • Wampongeza kwa namna anavyokiimarisha Chama Cha Mapinduzi na msimamo wake wa kutaka Viongozi kuwa karibu na wananchi

 Wakazi wa jimbo la Kibakwe wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Kibakwe stendi,Katibu Mkuu aliwataka viongozi wanaosimamia sheria kuzingatia wananchi wa kawaida na kuwashirikisha kwenye jambo linalowagusa kwenye shughuli zao za kila siku kwani kufanya hivyo kutawasaidia wananchi hao kuishi maisha yao na pia kuinua uchumi wa eneo husika.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Stendi ya Kibakwe,jimbo la Kibakwe wilaya ya Mpwapwa,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama mkoa wa Dodoma akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wakazi wa Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe na kuwataka wana CCM kuchagua viongozi wanaowataka na kusema wilaya au mkoa hawataka jina la mtu yeyote aliyechaguliwa na wananchi.
 Wananchi wa Kibakwe wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wao.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa jimbo la Kibakwe wilayani Mpwapwa na kuwataka vijana kuwa makini na wanasisa wasio na sera mbadala za kuwaletea maendeleo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe wilayani Mpwapwa.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa kijiji cha Luhundwa kata ya Rudi wilayani Mpwapwa ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi pamoja na kukiimarisha Chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmn Kinana akishiriki kupiga lipu darasa la shule ya sekondari Ikuyu,wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari kwenye shamba darasa la Kituo cha Kilimo, Taaluma na Mwasaliano kilichopo Kibakwe, wilayani Mpwapwa mkoa wa Dodoma.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnaye akisoma kibao chenye maelezo yanayohusu aina ya mbegu ya mahindi iliyopandwa na namna ya kuitunza kwenye Kituo cha Kilimo, Taaluma na Mwasaliano kilichopo Kibakwe

Katibu Mkuu wa CCM akipata maelezo ya namna ya kutumia vifaa vya kulimia alipotembelea Kituo cha Kilimo, Taaluma na Mwasaliano kilichopo Kibakwe wilayani Mpwapwa.
PICHA ZAIDI
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.