Monday, March 2, 2015

RAIS KIKWETE AONGOZA WAKAZI WA DAR ES SALAAM KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU KAPTENI JOHN KOMBA

 Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Kapteni John Komba likiwa limebebwa kuelekea kwenye jukwaa maalum kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Familia ya Marehemu Kapteni John Komba ikiwa imesimama tayari kuupokea mwili wa marehemu kwenye viwanja vya Karimjee.
 Ni huzuni kubwa kwa familia ya marehemu.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa pamoja na Makamu wa Rais Ghalib Bilal (kushoto) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee ambapo mwili wa Marehemu Kapteni John Komba uliagwa na Viongozi mbali mbali na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma salaam za rambi rambi kwa niaba ya CCM na wanachama wake wakati wa kumuaga marehemu Kapteni John Komba.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza na   Makamu wa Rais Ghalib Bilal kwenye viwanja vya Karimjee ambapo mwili wa Kapteni John Komba ulikuwa unaagwa .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  akiimba wimbo maalum wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba aliyefariki tarehe 28 februari 2015 jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wa CCM pamoja na wanamuziki wa muziki wa dansi wakiimba kwa pamoja nyimbo maalum wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa heshima ya mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba .
 Mzee Yusuf Makamba akifuta machozi wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba
 Kada wa CCM na Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba
 Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni CCM Dk. Mohamed Seif Khatib akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba
 Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa Bernard Membe akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba
 Viongozi na wananchi kutoka sehemu mbali mbali wakiwa kwenye foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba kwenye viwanja vya Karimjee.
Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Arusha Mheshimiwa Catheline Magige akiondoka eneo la tukio baada ya kumaliza kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu Kapteni John Komba.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.