Tuesday, March 24, 2015

KINANA : VIONGOZI WALIOKUWEPO MADARAKANI WAACHWE WAMALIZE MUDA WAO

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Moshi Ndugu Novatus Makunga wakati wa mapokezi kwenye kijiji cha Mikocheni ambapom Katibu Mkuu wa CCM alipita kuwasalimia wananchi wa kijiji hicho.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili eneo la mkutano kwenye kijiji cha Mikocheni, kata ya Arusha Chini.
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Moshi Vijijini Mzee Gabriel Massenga akihutubia wananchi wa kijiji cha Mikocheni ambapo aliwaambia anayofuraha kukutana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanakwani alikuwa mmoja wa wanafunzi wake kwenye shule ya sekondari ya Old Moshi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya CCM Ndugu Omari Mnaso ambaye alikuwa Katibu Tawi wa Chadema Mikocheni lakini ameamua kujiunga rasmi na CCM
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiingia kwenye eneo la ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro, pamoja nae ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kulia) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Juma Idd.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kwenye ngoma za kitamaduni wakati wa mapokezi kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Kilimanjaro.
 Shamba la Mpunga lililopo Mabogini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki uvunaji wa mpunga kwenye skimu ya umagiliaji ya Lower Moshi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mwenyekiti wa Halmashauri Ndugu Moris Makoi (katikati) na Mkurugenzi wa Halmashauri Ndugu fulgence Mponji mara baada ya kutembelea na kushiriki uvunaji mpunga kwenye skimu ya umwagili iliyopo kijiji cha Mabogini.
 Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Ndugu Cyril Chami akihutubia wananchi wa kijiji cha Chekereni kata ya Mabogeni.
Kata ya Mabogeni ina vijiji 8 na vyote vimeshinda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Jimbo la Moshi Vijijini lina Kata 16 ,shule za sekondari zilizojengwa ni 29.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Chekereni kata ya Mabogini
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi alipotembelea chuo cha KVTC
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda mti wa kumbukumbu kwenye chuo cha Ufundi KVTC.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mwanafunzi Elia PeterUlomi wa shule ya sekondari ya Somsom
 Mbunge wa Viti maalum Betty Machangu akihutubia wananchi wa Kibosho kwenye mkutano uliofanyika kwa Mangi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa  Kwa Mangi kata ya Kibosho Kati ambapo aliwaambia wananchi waache kujipitisha pitisha kugombea nafasi za uongozi kabla ya muda kuisha na kutangazwa.
 Zaidi ya wanachama 335 wajiunga na CCM kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana( katikati) pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa kwenye picha ya pamoja na vitukuu vya Mangi Sina, Kibosho ya Kati.
Hii nyumba ya Mangi sina ipo tangia mwaka 1890.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.