Sunday, March 8, 2015

KINANA : KATIBA MPYA IKIPITA TANZANIA KUWA YA KWANZA DUNIANI KWA KUWA NA NAFASI ZA UWAKILISHI YA HAMSINI KWA HAMSINI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi wa CCM wilaya ya Chamwino mara baada ya kuwasili kwenye shamba la Zabibu Chinangali II.
 Zabibu zikiwa zimestawi vizuri.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakulima katika mradi wa kilimo cha Zabibu kwenye kijiji cha Chinangali II wilaya ya Chamwino.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipuliza dawa ya kuua wadudu wanaoshambulia zabibu kwenye shamba la mradi wa kilimo cha zabibu katika kijiji cha Chinangali II wilayani Chamwino.

 Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mheshimiwa Farida Salum Mgomi akipulizia dawa ya kuua wadudu zabibu kwenye shamba la zabibu Chinangali II, kulia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM kupitia Vijana  Ndugu Deo Ndejembi.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili ukumbinitayari kushiriki mkutano maalum wa Jimbo la Chilomwa,wilayani Chamwino.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchimba shimo la choo cha shule ya msingi Kikwete iliyopo Chamwino mkoani Dodoma.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chilomwa kabla ya kushiriki ujenzi wa zahanati.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Chilomwa wilayani Chamwino ikiwa sehemu ya ziara ya kujenga na kuimarisha chama.
 Kila kona kila mtu anapendeza na fulana za CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiingia kwenye uwanja wa mikutano kwa staili ya aina yake kijijini Majereko wilaya ya Chamwino.
 Wananchi wakiangalia vikundi vya ngoma vikitumbuiza.
 Wasanii wa Kikundi cha ngoma kutoka Chamwino wakionyesha burudani ya ngoma ya Kigogo kabala ya kuanza kwa mkutano wa hadhara ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Marejeko kwenye viwanja vya shule ya msingi Marejeko na kutoa salaam maalum katika siku ya wanawake duniani kwa kuipongeza serikali kwa kutoa nafasi nyingi kwa wanawake.
 Wananchi wakisikiliza hotuba za viongozi
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa Majereko ambapo alitoa salaam za Chama Cha Mapinduzi za kuwatakiwa wanawake heri ya siku yao,aliwaambia haki za wanawake wa Tanzania zipo salama chini ya CCM.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Chiku Galawa akiwasalimu wananchi wa Marejeko wilaya ya Chamwino.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.