Monday, March 16, 2015

KINANA AWEKA HISTORIA KARATU

  • ZAIDI YA WANACHAMA 324 KUTOKA CHADEMA WAJIUNGA NA CCM
  • AIVUNJA NGOME KUU NA YA MWANZO YA CHADEMA QURONG'IDHA
  • WANANCHI WAKIRI WALIFANYA MAKOSA KUUCHAGUA CHADEMA
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KARATU IMEJAA UBADHILIFU
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Karatu kwenye uwanja wa mikutano wa Mazingira Bora.
Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kujenga na kukiimarisha Chama mkoa wa Arusha pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Karatu mjini na kuwaambia wapinzani muda wao umekwisha Karatu mjini kwani hamna walichofanya kwa zaidi ya miaka 15 waliyokaa madarakani.
 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda akiwa haamini macho yake jinsi wananchi wa Karatu wanavyojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM.
 Wananchi wa Karatu wakishangilia kwa nguvu mkutano wa CCM
 Wingi huu wa watu wanaashiria kuwa na matumaini na CCM zaidi mjini Karatu
 Wananchi wa Kijiji cha Mang'ola wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,ambapo walimpa malamikoyao juu ya uongozi wao kufanya maamuzi bila kushirikisha wananchi,kubuni miradi hewa na kula fedha.
 Wananchi wa Kijiji cha Mang'ola wilaya ya Karatu wakionyesha ishara za kukubaliana na Katibu Mkuu wa CCM.
 Wananchi wakiwa juu ya mti ili waweze kumuona vizuri Katibu Mkuu wa CCM wilaya ya Karatu kijiji cha Mang'ola.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na wananchi kuelekea kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Mang'ola wilaya ya Karatu
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirki kupanda vitunguu pamoja na wananchi katika shamaba la Mang'ola Barazani.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwenye maeneo ya Mang'ola barazani mara baada ya kutemebelea miundo mbinu ya umwagiliaji ambayo imelalamikiwa na wananchi hao kwa kuwa ni mibovu na haiwasaidii wananchi hao.
Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi kutoka Chadema kata ya Baray wilaya ya Karatu Juliana Israel akitangaza kujiunga na CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Mbuga Nyekundu kata ya Baray.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kata ya Baray
 Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Baray wilaya ya Karatu
 Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Flora Lazari Zelothe akisalimia wananchi wa kata ya Baray
Wananchi wa Karatu wakionyesha kufurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana.
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.