Wednesday, March 25, 2015

KINANA AWATAKA WANANCHI WA VUNJO KUCHAGUA CCM

  • Awaambia ushabiki wa kisiasa unarudisha nyuma maendeleo ya Vunjo
  • Awataka wana CCM kushikamana na kuwa kitu kimoja
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Oria,Kata ya Kahe Magharibi,Jimbo la Vunjo ikiwa muendelezo wa ziara za kuimarisha chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Oria kabla ya kuona mradi wa vijana wa ufatuaji matofali ya bei nafuu kwenye ziara yake ya jimbo la Vunjo.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali kwenye mradi wa vijana wa kijiji cha Oria ,kata ya Kahe Magharibi.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Uchira kata ya Kirua Vunjo Kusini ikiwa sehemu ya kukagua na kuimarisha uahai wa chama.

 Wananchi wakijumuika wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Uchira,kata ya Kirua Vunjo kusini.


 Kikundi cha wakina mama wa Uchira ambao wanaendesha vikoba wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Msafara wa  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukiwasili Himo Wanamuziki wa Bendi ya Lokaa wakijiachia barabarani wakati wa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM kwenye kata ya Makuyuni,Himo.
 Katibu Mkuu wa CCM akinunua ndizi barabarani Himo wakati akielekea kwenye uwanja wa mkutano
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa mkutano wa CCM jimbo la Vunjo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wazee wa Himo wakati akiwasili kwenye uwanja wa mkutano.
 Wananchi wakisikiliza viongozi wao kwenye mkutano wa hadhara.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye uwanja wa polisi Himo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa muda umefika sasa wa kufanya maamuzi ya msingi kwa kuchagua kiongozi anayeweza kuleta maendeleo katika Jimbo la Vunjo.
  Wananchi wa Kata ya Makuyuni wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye aliwaambia kwa miaka mingi sasa jimbo la Vunjo limekuwa linarudishwa nyuma na ushabiki wa kisiasa na kuwataka wananchi hao kufanya maamuzi sahihi mwaka huu kwa kuichagua CCM

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa kata ya Makuyuni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyiaka kwenye viwanja vya polisi himo na kuwaambia wananchi hao wapinzani hawana tena ubavu wa kuongoza kwani kwa zaidi ya miaka mingi sasa wamepata nafasi na hamna walichokifanya kwa wananchi hao wa jimbo la Vunjo.
 Kijana kutoka chama cha Chadema membeck Kaigarula akikabidhi kadi ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanana kutangaza rasmi kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Himo.


 Billy Francis akihutubia wakazi wa Himo mara baada ya kutangza rasmi kuondoka Chadema na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwana vya polisi Himo na kuhutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.