Saturday, March 21, 2015

KINANA ATEMBELEA VIWANDA VYA GENERAL TYRE NA KILTEX

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimwaga saruji wakati wa kushiriki ujenzi wa barabara ya Olorieni kwa kiwango cha Lami ikiwa sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiendesha gari maalum la kuchonga barabara wakati wa ujenzi ya barabara ya Olorieni,Arusha mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiingia kwenye kiwanda cha matairi cha Arusha kinachojulikana kama General Tyre.
 Kiwanda cha Matairi cha General Tyre
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mitambo ya kiwanda cha matairi cha General tyre kinachotegemewa kuanza kazi mwishoni mwa mwaka huu ambapo serikali imeamua kufufua kiwanda chini ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC).

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na viongozi wengine wa CCM mkoa wa Arusha nje ya majengo ya kiwanda cha nguo cha Kiltex ambacho kimefungwa na mmiliki wake kukimbia baada ya kugundulika kiwanda chake hakifanyi kazi,amegeuza ghala na kuondoa mashine zote.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine wa CCM wakiwa nje ya geti la kiwanda cha Kiltex baada ya mmiliki wake kukimbia
 Mlinzi mkuu wa kiwanda cha Kiltex akiongea na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kiwanda hicho kufungwa na mmiliki kukimbilia Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwenye kiwanda cha Kiltex.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.