Sunday, March 15, 2015

KINANA AMALIZA ZIARA WILAYA YA NGORONGORO

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Arash wilaya ya Ngorongoro,ambao  walimueleza Katibu Mkuu wa CCM kero zao,ikiwemo tatizo la kuchomewa makazi yao na askari wa hifadhi pamoja na tatizo la maji.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa mkutano na Baraza la wafugaji,Viongozi wa Kata na Viongozi wa Kimila.
 Wajumbe wa baraza la wafugaji,viongozi wa kata na viongozi wa kimila wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro Ndugu Metui Olle Shaudo akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akishiriki kupaka rangi nyumba ya Mganga iliyojengwa na wanakijiji cha Bulati,wengine ni Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro Ndugu Saning'o Ole Telele(kulia) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Onesmo Ole Nangole.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Arusha akisalimia wakazi wa kijiji cha Bulati.
Katibu Mkuu wa CCM akizungumza na wanakijiji cha Bulati
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiongozana na wananchi kuelekea kwenye kijiji cha Nainokanoka ambapo mkutano wa hadhara ulitegemewa kufanyika.
 Katibu Mkuu wa CCM akikaribishwa kwa ngoma za kiasili za Kimaasai kabla ya kuanza kwa mkutano katika kijiji cha Nainokanoka
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya kuanza kuhutubia wananchi wa kijiji cha Nainokanoka, Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mama wa Kimaasai akifuatilia mkutano kwa makini
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Nainokanoka,Ngorongoro mkoani Arusha.
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Nainokanoka ikiwa sehemu ya ziara za kuimarisha  Chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi Mbuzi kwa mmoja wa mama wajane,ambapo mbuzi zaidi ya 2274 walitolewa na Baraza la wafugaji wa Ngorongoro kwa wanawake wajane, walemavu na wasiojiweza.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na vijana wa Kimaasai mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.