Saturday, March 7, 2015

KINANA AKUTANA NA SHIRIKISHO LA WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU YA JUU DODOMA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa nje ya ukumbi wa NEC maarufu kama white house mjini Dodoma tayari kwa kukutana na wanafunzi wa Shirikisho la vyuo vya elimu ya juu mkoani Dodoma.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu mkoani Dodoma kabla ya kuingia kwenye mkutano kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC maarufu kama White House,CCM makao makuu Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia na Viongozi mbali mbali wa CCM mkoa wa Dodoma.
 Katibu Mtendaji wa Shirikisho a Vyuo vya Elimu ya Juu nchini Ndugu Christopher Ngubiagai akizungumza wakati mkutano wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Dodoma.
 Wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu wakisikiliza kwa makini hoja mbali mbali zilizokuwa zikijadiliwa wakati wa mkutano huo.
 Judith Haule kutoka Chuo cha Mipango Dodoma akizungumzia masaula ya ajira na changamoto zake na mfumo wa elimu unaosababisha watu waamini katika kuajiriwa zaidi na si kujiajiri.
 Thomas Mathias kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma akizungumza kwenye mkutano wa shirikisho la vyuo vya elimu ya juu Dodoma na kuzungumzia masauala mbali mbali yanayohusu mikopo na kuwawezesha wanafunzi wengi kupata fursa ya kusoma elimu ya juu nchini.
 Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu wakisimama kwa dakika moja kumuombea Marehemu Kapteni John Komba aliyefariki dunia tarehe 28 Februari 2015 mjini Dar es salaam.

 Kimario Idd kutoka chuo cha mtakatifu John akitoa ushauri kwa Chama na Viongozi wengine wawajibike katika kuipa nguvu Shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania.
Kalegele Mkuyu kutoka chuo cha CBE akihimiza viongozi wa CCM hasa wabunge kujenga utamaduni wa kukutana na wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu wa mkoani Dodoma ambapo alisisitiza wanafunzi wa elimu ya juu kuja na mawazo mapya yatayoweza kuimarisha uchumi wa nchini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu Dodoma na kuwaambia sifa kubwa na muhimu kwa kiongozi katika nchi ni uadilifu,aliwaambia ukiwa kiongozi lazima uwe mwadilifu ili watu wakuamini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mikono na viongozi wa vijana wasomi waliomaliza vyuo vikuu na kuunda kikundi  cha New Generation Network ambao walikabidhiwa cheki ya shilingi milioni 10 iliyotoka kwenye mfuko wa maendeleo ya vijana waWizara ya Habari ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo
 Mohamed Masoud Ikome Afisa Mipango na fedha wa kikundi cha New Generation Network akionyesha cheki ya shilingi milioni 10 liyotoka kwenye mfuko wa maendeleo ya vijana waWizara ya Habari ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo.
Mohamed Masoud Ikome Afisa Mipango na fedha wa kikundi cha New Generation Network akitoa salaam za shukrani mara baada ya kukabidhiwa cheki ya shilingi milioni 10 liyotoka kwenye mfuko wa maendeleo ya vijana waWizara ya Habari ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.