Friday, March 6, 2015

KINANA AITEKA WILAYA YA KONGWA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Jimbo la Kongwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mkoka,wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ikiwa sehemu ya muendelezo wa ziara zake za kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2010.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mkoka wilayani Kongwa na kuwaambia moja ya sifa muhimu na ya kipekee kwa kiongozi anayefaa kuongoza wananchi ni Uadilifu.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni wa heshima, Kimbisa aliwaambia wana CCM kuwa Dodoma itakuwa mfano katika kutenda haki.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mkoka wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma ambapo aliwaambia wananchi hao CCM ni Chama pekee chenye kujali Watanzania kinachosimamia na kuitunza amani iliyokuwepo.
 Mbunge wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha Chama.
 Kikundi cha ngoma cha Faru kikitumbuiza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Aliyekuwa Katibu Mwenezi Kata ya Ngomae na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema wilaya ya Kongwa Ndugu Makang'ata Nyanje akitangaza kurudi CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mkoka kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Aliyekuwa Katibu Mwenezi Kata ya Ngomae na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chadema wilaya ya Kongwa Ndugu Makang'ata Nyanje akimkabidhi kadi yake ya Chadema Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mkoka wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamaba la kijiji pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mheshimiwa Bituni Msangi na wananchi wengine katika kata ya Iduo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Kata ya Mlali wakati wa uzinduzi wa kituo cha maji.
 Wananchi wa Mlali wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati wa uzinduzi wa kituo cha maji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji kwenye kituo cha Mlali wilaya ya Kongwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi. Subiraga Bukuku mkazi wa kijiji cha Mlali mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji hicho.
 Mwenyekiti wa CCM Ndugu Adam Kimbisa akishiriki ufyatuaji wa matofali ya kujengea mabweni ya watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mlali B akishirikiana na Mkuu wa mkoa  wa Dodoma Ndugu Chiku Galawa.
 Mbunge wa Kongwa Ndugu Job Ndugai akieleza namna alivyopata tabu kushawishi ujenzi wa bweni kwa watoto wenye mahitaji maalum.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na wasanii wa kikundi cha ngoma cha Amani kwenye kijiji cha Njoge kata ya Mlali wilaya ya Kongwa.
 Mbunge wa Jimbo la Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Job Ndugai akihutubia wakati wa mkutano wa kuwasalimia wananchi wa kijiji cha Njoge na kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushiriki ujenzi wa Zahanati.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Njoge kata ya Mlali mbele ya jengo la la zahanati ya kijiji linalojengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na serikali.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakimpa mkono wa pongezi kwa kazi nzuri anayofanya jimboni kwake Mbunge wa Jimbo la Kongwa Ndugu Job Ndugai
 Baba akimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanahuku akiwa amembeba binti yake.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasikiliza wananchi wa kijiji cha Songambele ambao walimueleza Katibu Mkuu kuwa wana tatizo kubwa la Umeme kutofika kwenye Hospitali,Visima vya maji na Shule.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakijibu baadhi ya maswali alioulizwa na wananchi wa kijiji cha Songambele waliomsimamisha njiani wakati akielekea Mkoka kwenye mkutano wa hadhara.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.