Monday, March 30, 2015

KINANA AITEKA TARAKEA

  • Azitaka mamlaka husika kurahisisha ufanyaji biashara kwa watu wa mipakani
  • Awaambia vijana waache siasa za kishabiki kwani hazina tija
  • Mwenezi wa Chadema wilaya ya Rombo ajiunga na CCM
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Tarakea wilayani Rombo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Tarakea Polisi.

Katibu Mkuu wa CCM anaendelea na ziara za kujenga na kuimarisha Chama mkoani Kilimanjaro pamoja na kukagua, kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
Katika ziara yake ya leo wilayani Rombo ,Katibu Mkuu alishiriki shughuli mbali mbali ,zikiwemo kufungua ofisi ya chama ya wilaya, kukabidhi Bima ya afya kwa vijana 900 wa boda boda,Kukabidhi mikataba na hundi ya vikundi 2o vya wanawake wajasiriamali.
 Wakazi wa Tarakea wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye viwanja vya polisi Tarakea.
Wakazi wa tarakea wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jioni ya leo.
 Wananchi wa Tarakea wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana bila kujali mvua iliyokuwa inawanyeshea.

Bw. John Tarimo aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Rombo na Katibu wa Mbunge wa jimbo hilo Mh. Joseph Selasini akitangaza rasmi kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Polisi mjini Tarakea
ZIARA YA KINANA WILAYA YA ROMBO

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vikundi vya utamaduni wakati akiwasili kwenye ofisi ya CCM wilaya ya Rombo.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka wilaya ya Rombo Ndugu Evod Mmanda akiwasalimu wananchi wa Rombo waliofika kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Mkuu wa Wilaya ya Rombo akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi  kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Rombo nje ya ofisi ya CCM wilaya na kuwaambia CCM imejiimarisha zaidi na itaendelea kujiimarisha na kuwataka wananchi hao kuendelea kukiamini chama chao chenye sera inayoeleweka.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana akiwahutubia wananchi wa Rombo kabla ya kufungua ofisi ya CCM wilaya ya Rombo ambapo aliwaambia wananchi hao kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo kwa wananchi na kutaka kuacha ushabiki wa kisiasa ambao hauwanufaishi wao zaidi ya wabunge waliowachagua ambao wanakaa madarakani bila kuwasaidia wananchi,alisema kuna wabunge hawafanyi mikutano,hawachangii maendeleo katika mfuko wa jimbo, wanapinga bajeti ya maendeleo hawatoi taarifa za huduma mbali mbali za kijamii ,wala hawasaidii katika miradi mbali mbali ya wananchi ikiwa umeme,maji ,barabara na afya ni vyema wakaachwa na kupisha kiongozi anayejua na kutambua matatizo ya wananchi.
 Jiwe hili la msingi la ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya liliwekwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye mwezi Oktoba 2012

Jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo la ofisi ya CCM wilaya ya Rombo ambalo limewekwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mwezi Machi 2015.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi bima ya afya Ndugu Eugen Thomas Silayo ambaye ni dereva wa boda boda.
 Vikundi vya wajasiriamali kutoka wilaya ya Rombo katika picha ya pamoja wakiwa wameshikilia mikataba na hundi walizokabidhiwa leo.


 Kaburi la pamoja la wanafunzi 38 wa Shule ya Sekondari Shauritanga waliopoteza maisha yao kwenye ajali ya moto iliyotokea mwaka 1994 .

020
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa heshima zake katika kaburi la pamoja la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Shauritanga waliofariki katika ajali ya moto mwezi juni mwaka 1994.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ambapo aliwaambia CCM ndio chama pekee chenye utaratibu wa kila jambo lake lipo kwenye kanuni,katiba na sheria hivyo kuwataka wajumbe hao kuzifuata .

 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Rombo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya namna uzalishaji unafanyika kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kutengeneza vinywaji ya Bellaview Fresh Fruits Processing Industry Ndugu Shanel John Ngowi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Bellaview Fresh Fruits Industry kilichopo Rombo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuvuta waya wa umeme kwenye mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Kirongo Samanga ikiwa sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.


 Mafundi wa Tanesco wakifunga njia ya umeme katika kijiji cha Kirongo Samanga wilayani Rombo ambapo zaidi ya asilimia 80 ya vijiji katika wilaya hiyo vitapata umeme katika awamu ya pili na vilivyobaki vitapata umeme katika awamu ya tatu.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya mradi wa maji katika kijiji cha Kahe kutoka kwa Injinia wa maji wilaya ya Rombo Ndugu Andrea Sawake Tesha.
Mradi huo wa maji umegharimu shilingi milioni 524 ,lina ujazo wa lita 250,000 na utahudumia wakazi 7,763 wa kijiji cha Kahe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiruka baada ya kukagua tanki la maji katika mradi wa maji safi na salama kijiji cha Kahe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Kahe ambapo aliwaambia wachague viongozi wenye kufanya kazi na wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufunga bomba tayari kwa uzinduzi wa maji safi na salama kwa wananchi wa kijiji cha Kahe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji ikiwa sehemu ya uzinduzi wa huduma ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Kahe pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Lembris Marangushi Kipuyo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi. Petronila Jakob kama ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma ya maji katika kijiji cha Kahe.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA


Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.