Wednesday, March 4, 2015

BAADA YA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO KINANA AANZA KAZI YA KUIMARISHA CHAMA MKOANI DODOMA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) akiongozana na  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakipokelewa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa.
Katibu Mkuu aliwasili Dodoma leo asubuhi akitokea mkoani Ruvuma ambapo alishiriki mazishi ya Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba.
 Bango lenye ujumbe wa kumkaribisha Kinana mkoani Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu na vijana wa chipukizi mara wakati wa mapokezi kwenye ofisi za CCM wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.
 Vijana wa Chipukizi wa CCM wilaya ya Mpwapwa wakiimba nyimbo ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wilayani hapo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa wakati wa mapokezi kwenye ofisi za CCM wilaya.
 Wasanii wa kikundi cha ngoma cha Mpwapwa wakitumbuiza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM kwenye ofisi za CCM wilaya ya Mpwapwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi waliojitokeza kumpokea nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Mpwapwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi waliojitokeza kumpokea kwenye ofisi za CCM wilaya ya Mpwapwa ikiwa sehemu ya ziara yake ya kujenga na kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimia wananchi waliojitokeza kuwapokea kwenye ofisi za CCM Mpwapwa.
Sare za Chama Cha Mapinduzi zikiwa katika kila aina ya ubunifu nje ya jengo la CCM wilaya ya Mpwapwa ambapo wananchi,wapenzi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi walikuwa wanajinunulia.
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.