Saturday, March 28, 2015

ANNE KILANGO AISHUKURU SERIKALI YA CCM KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI JIMBONI KWAKE


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mashine ya kupasulia mbao wakati alipotembelea chuo cha ufundi  Maore kilichopo kata ya Muheza, Same Mashariki.
Chuo hicho kitachukua wanafunzi 300.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi katika chuo cha ufundi Maore kata ya Muheza jimbo la Same Mashariki ikiwa sehemu ya ziara ya kujenga na kuimarisha chama.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati alipotembelea chuo cha ufundi Maore,wengine pichani ni Padri Everest Abeid,Padri Japhet Njaule (kulia) na Padri Moses Mbwambo ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Anne Kilango Malecela
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusuka nondo kwenye daraja la Mang'a katika kijiji cha Mang'a Myamba, Same Mashariki.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amesimama kwenye mto Mang'a.
  Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Anne Kilango Malecela akizungumza na vyombo vya habari kushukuru serikali ya Chama Cha Mapinduzi kujenga daraja la Mang'a katika kijiji cha Goha mbele ya  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akiweka shada la maua pamoja na Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Ndugu Anne Kilango Malecela(katikati) ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) kwenye makaburi ya watu waliofariki kwa mafuriko na maporomoko ya mawe yaliyotokea kiijiji cha Goha kitongoji cha Mang'a.
 Ujumbe wa kijijiwe kimoja kijiji cha Goha huko Same Mashariki.
 Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Ndugu Anne Kilango Malecela akielezea changamoto ya mtaji wa kukiwezesha kiwanda cha kusindika Tangawizi kuweza kufanya uzalishaji bora kwa  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea kiwandani hapo Mang'a Myamba ,Same Mashariki.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Mang'a Myamba nje ya kiwanda cha kusindika Tangawizi ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia namna Tangawizi inavyoandaliwa kusindikwa kwenye kiwanda cha usindikaji tangawizi kilichopo Mang'a Myamba.
 Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela na Mbunge wa Viti Maalum Wanawake mkoa wa Kilimanjaro Betty Machangu wakiteta jambo na  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuingia kwenye mkutano Mkuu wa Jimbo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanachi wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa mkutano Ndungu ,Same Mashariki.
 Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano huo wa hadhara.
 Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki Ndugu Anne Kilango Malecela akihutubia wananchi wa Ndungu kwenye mkutano wa hadhara wa CCM
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape akihutubia wakazi wa Same Mashariki na kuwataka kuendelea kuamini Chama Cha Mapinduzi kwani vyama vingi vya upinzani havina uwezo wa kuongoza kutokana na kukosa sera mbadala kwa maendeleo ya wananchi.
 Wananchi wakifuatilia mkutano
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Same Mashariki ambapo alisema CCM itasimama imara kutetea haki za wanyonge nchi nzima na kuwataka viongozi na wana CCM kwa jumla wawe mstari wa mbele katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM 2010.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.