LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 26, 2015

RIDHIWANI KIKWETE ALIPOFIKA OFISI ZA UWAKILISHI WA KUDUMU WA TANZANIA KATIKA UMOJA WA MATAIFA, NEW YORK

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze  na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya  Chama cha  Mapinduzi Mhe. Ridhiwani Kikwete akiwa  katika picha ya   pamoja na  Muwakilishi wa Kudumu wa Jamburi ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako  Manongi  (kushoto) na  Naibu Mwakilishi wa  Kudumu,  Balozi Ramadhan Mwinyi. Mhe Ridhiwani Kikwete ( Mb)  alikuwa Jijini New York kwa ziara ya kikazi ambapo pia  alikuwa mgeni  rasmi  katika  hafla ya  miaka 38 ya  kuzaliwa kwa  Chama cha Mapinguzi iliyoandaliwa na Tawi la CCM New York na vitongoji vyake.
Mhe. Ridhiwani Kikwete ( Mb) akiwa  katika picha ya pamoja na  Mabalozi   na  baadhi ya  maafisa wa Uwakilishi wa  kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. Mhe.  Ridhiwani Kikwete  pamoja na  kuhudhuria hafla ya   CCM kutimiza miaka 38 pia alipata fursa ya kufika katika Ofisi za Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika  Umoja wa Mataifa, fursa aliyoitumia  kubadilishana  mawazo  na   Maafisa wa Uwakilishi.  Na Mpigapicha Maalum, New York

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages