LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 22, 2015

MKUTANO WA 16 WA KAWAIDA WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI NAIROBI,KENYA, KATIKA PICHA



 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi jijini Nairobi kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kuhudhuria mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwindikiza na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi walipokutana jijini Nairobi kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kuhudhuria mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakipigiwa wimbo wa taifa wa Tanzania baada ya kuwasili  kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kuhudhuria mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015. Kulia ni Naibu Rais wa kenya Mhe. William Samoei Ruto
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wakisimama kwa wimbo wa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki   kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wakiwa meza kuu  kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya baada ya kupokea kijiti cha kuongoza jumuiya hiyo wakati wa   mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Jumuiya hiyo Dkt Harrison Mwakyembe akiwasilisha ripoti ya mwaka ya baraza hilo   mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Bango la wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Jumuiya baada ya kukabidhiwa  ripoti ya mwaka ya baraza hilo   mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga Rais Paul Kagame wa Rwanda aliyekwemnda kumuomba udhuru ili kuondoka mapema kabla ya kumalizika kwa  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Jaji Geoffrey W. M. Kiryabwire akiongozwa kuelekea jukwaani kula kiapo kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimpongeza Jaji Audace Ngiye kutoka Burundi baada ya kula  kiapo  kuwa Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimpongeza Mhe Liberag Mpfumukeko kutoka Burundi baada ya kuteuliwa kuwa Nibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mshariki  wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Waziri wa Ushirikiano wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Jumuiya hiyo Dkt Harrison Mwakyembe akishauriana jambo na  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika MasharikiJoyce Mapunjo wakati wa mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Wanafunzi washindi wa Insha wakisubiri kupokea tuzo zao katika  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda akipungia mkono wajumbe walioko Kampala baada ya Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuzindua mfumo wa kisasa wa mawasiliano ya moja kwa moja kwa njia ya video uitwao Telepresence katika  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Ujumbe wa Tanzania katika  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015, Kutoka kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mhe Bernard Membe, WAZIRI wa nchi ofisi ya rais anayeshughulikian utawala bora  Mhe. George Huruma Mkuchika, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe  George Mcheche Masaju, Waziri wa Fedha, Mhe, Saada Mkuya Salum na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Lazaro Nyalandu
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika kilele cha   mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta wa kenya na Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini baada ya  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Uhuru Kenyatta wa kenya, Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi na Naibu Rais wa kenya Mhe. William Samoei Ruto  baada ya  mkutano wa 16 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Afrika Mashariki February 20, 2015. Picha zote na IKULU

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages