Monday, February 23, 2015

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YAWAKUMBUKA WAHANGA WA JANGA LA MVUA 


Wakazi wa Mtaa wa Ilemi juhudi jijini Mbeya wakiwa tayari kukabidhiwa msaada huo.


Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Quip Mbeyela akizungumza katika makabidhiano ya Msaada huo.


Kaimu Mkurugenzi jiji la Mbeya Dkt Samwel Lazaro akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo kwa waathirika wa janga hilo.Picha na David Nyembe Fahari News
Na Emanuel Madafa,Mbeya
Halmashauri ya jiji la Mbeya imetoa  msaada kwa Wananchi   wa Mtaa wa Ilemi jijini Mbeya  kufuatia makazi yao kuharibiwa vibaya na mvua iliyoambatana na upepo mkali  hivi karibuni na kusababisha  athari kubwa kwa wananchi hao .

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Kaimu Mkurugenzi Halmshauri ya jiji la Mbeya Dkt Samwel Lazaro amesema baada ya kupata taarifa za janga hilo uongozi wa halmashauri hiyo ulikaa na kujadiliana namna ya kutoa msaada kwa waathirika hao.

Amesema katika majadiliano hayo uongozi huo  ulikubaliana na kuamua kutoa mchango wao ambao Sukari kilo 3 kwa kila kaya pamoja na Unga wa ugali mfuko mmoja wa kilo 10 na Maharagwe kilo 1.

Amesema pamoja na kutoa msaada huo lakini pia uongozi wa halmshauri hiyo umeanza mchakato wa kufanya tathimini
ili kutambua hali halisi ya uhalibifu huo.

Aidha Dkt Lazoro amesema kuwa kutokana na baadhi ya miundo mbinu ya shule ya Msingi Ilemi kuharibiwa kwa kuezuliwa mapaa yake pamoja na vyoo tayari mafundi wamekwisha anza utaratibu wa kufanya ukarabati kwa gharama za serikali pasipo kuwa husisha wananchi .

Mvua hizo zilizo nyesha hivi karibuni jijini hapa zilileta madhara hayo kwa kuharibu baadhi ya miundo mbinu ya shule ya msingi Ilemi pamoja na kuharibu makazi ya watu kwa kaya zaidi ya 38 na kupelekea wakazi hao kukosa mahali pa kuishi pamoja na kuhitaji msaada wa maradhi mbalimbali.
Mwisho.


Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.