Sunday, January 25, 2015

UZINDUZI WA SHEREHE ZA KUZALIWA KWA CCM KUTIMIZA MIAKA 38 WAFANA PEMBA Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akihutubia wakazi wa Chake Chake Pemba kwenye uwanja wa mikutano mkongwe Gombani ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa CCM inataka kuingia kwenye uchaguzi kukiwa na amani na mshikamano,alisema"muungano wetu ndio ngao yetu" na kusisitiza Demokrasia imeanzishwa na CCM kwa kukubali mfumo wa vyama vingi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Chake Chake ambapo alitoa pongezi kwa viongozi wa CCM Zanzibar wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti kwa kufanya kazi nzuri ya kuimarisha Chama.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Ndugu Vuai Ali Vuai akihutubia wananchi kwenye sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa mkongwe Gombani.
 Kikundi cha sanaa kikionyesha moja ya ngoma ya Msewe yenye asili ya visiwani Zanzibar kwenye sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 38 y kuzaliwa kwa CCM ,Gombani Pemba.
 Picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikionyeshwa juu wakati wa sherehe hizo.
 Waimbaji Utenzi wakiimba Utenzi Maalum wakati wa maadhimisho hayo
 Vijana wa Halaiki wa CCM wakiimba nyimbo za kuwaheshimu waasisi na viongozi wetu.
 Vijana wa Chipukizi wakiinua picha ya muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar na Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Sheikh Abeid Karume kwenye uzinduzi wa sherehe za kutimiza miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM
 Bendi ya Brassband ya Vijana wa CCM ikitumbuiza.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Hadija Abood akisalimia wananchi waliojitokeza kuhudhuria uzinduzi wa sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM,kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Gombani,Pemba.
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye sherehe za uzinduzi wa miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM ,zilizofanyika kwenye uwanja wa Gombani ,Chake Chake Pemba.
 Naibu Katibu Mkuu wa UWT Tanzania Zanzibar, Salama Aboud Talib akisalimia wananchi
 Wananchi wakishangilia wakati viongozi wao walipokuwa wanatoa salaam.
 Katibu wa NEC Itikadi na Unezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwasalimu wakazi waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa sherehe za kutimiza miaka38 ya kuzaliwa CCM kwenye uwanja wa mkutano Gombani.
Viongozi wakishiriki kuomba duo mara baada ya kumaliza mkutano wa uzinduzi wa sherehe za kutimiza miaka 38 tangia kuzaliwa kwa CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa Gombani,CaKeChake Pemba.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.