Tuesday, January 13, 2015

MTEMVU ANOGESHA SHEREHE ZA CCM KATA YA MIBURANI KUNYAKUA VIYO VYOTE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

 Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Miburani, Ali Kamtanda akitoa maneno ya utangulizi wakati mgeni rasmi katika sherehe ya Kata hiyo kuzoa mitaa yote mitano katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika hivi karibuni, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu alipowasili katika ukumbi wa CCM Kata ya 15, Temeke mjini Dar es Salaam leo.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (wapili kushoto) akiwa meza kuu na viongozi wengine alipowasili ukumbini kwenye sherehe hiyo
 Wananchi wa Kata ya Miburani waliohudhuria sherehe hiyo wakiwa wamesimama ukumbini kumlaki Mtemvu
 Wadau waliohudhuria sherehe hizo wakishangilia Mtemvu alipoingia ukumbini kwenye sherehe hiyo
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana mkoa wa Dar es Salaam, akiwasili ukumbini na kupokea na Mtemvu
 Katibu wa CCM Kata ya Miburani akitoa neo la utangulizi kwenye sherehe hiyo
 Katibu wa Mbunge wa Temeke, Kaka Ally akisalimia wadau kwenye sherehe hiyo
 Mzee wa Temeke,  Tatu Farijala akimkumbatia Mtemvu kabla ya kumvalisha joho la Ukamanda wa CCm Kata ya Miburani wakati wa sherehe hiyo
 Tatu Farijala akimvalisha joho hilo la Ukamanda
 Mzee Logatus Ngonyani akimvisha kofia rasmi Mtemvu wakati wa kumtawaza kuwa Kamanda wa CCM wa Kata ya Miburani wakati wa sherehe hiyo.
 Mzee Methew Hoza akimkabidhi mtemvu mkuki ikiwa ni ishara kumthibitisha kutawazwa kuwa Kamanda wa CCM Kata ya Miburani
 Mtemvu akionyesha ngao na mkuki alivyokabidhiwa na wazee wa Kata ya Miburani Temeke baada ya kumtawaza kuwa Kamanda wa CCM wa Kata hiyo wakati wa sherehe hiyo
 Mtemvu akiwa na viongozi na wazee baada ua kuvishwa ukamanda
 Burudani ya ngoma kutoka kwa kikundi cha vijana wa Kata ya Miburani ikihanikiza wakati wa sherehe hiyo
 Kinana wa kikundi hicho akionyesha uhodari wake wa kuchezea moto kwa kuuingiza mdomoni wakati wa sherehe hiyo
 Kijana huyo akionyesha umahiri wake wa kuchezea moto mbele ya meza kuu
 Mtemvu akizungumza wakati wa sherehe hizo, ambapo alitoa pongezi nyingi, lakini akawataka wa CCM kuongeza mshikamano zaidi kwa ajili ya kuhakikisha katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu inashinda, badala ya kuingia katika fitina na malumbano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yataangamiza chama
 Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika kata ya Miburani wakisalimia wananchi walipotambulishwa kwenye sherehe hiyo
Mtemvu akiwa na Wenyeviti wa Serikali za mitaa walioshinda kwa tiketi ya CCM katika kata hiyo ya Miburani wakati wa sherehe hiyo ya kupongeza ushindi amewataka viongozi hao kufanya kazi za wananchi badala ya kujisahau na kuanza kufanya shughuli kwa ajili ya maslahi ya mtu au wao binafsi
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.