Tuesday, January 27, 2015

KINANA AWATAKA WANACCM KUWEKA VIONGOZI WAZURI PEMBA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mbunge wa Viti Maalumu Pemba Maida Hamad Abdala mara baada ya kuwasili katika wilaya ya Wicheweni ikiwa siku ya pili ya ziara yake kwenye mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wa maskani ya Mnarani Tuheshimiane  ambao vijana zaidi ya 105 waliamua kujiunga na CCM kutoka vyama vya CUF na ADC,Vijana hao walimueleza Katibu Mkuu wamekuwa wakinyanyasika na kutengwa kwa uamuzi wao wa kujiunga na CCM,Makangale,Micheweni Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Afisa Mkuu wa Idara ya Umwagiliaji Mbarouk Ali Mgau wakati alipotembelea bonde la Koowe kushiriki ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi yathiathiri mashamba ya mpunga, Koogwe Wingwi,Micheweni Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi alioongozana na wa Chama na Serikali wilaya ya wete wakipita kukagua maendeleo ya ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi katika bonde la mpunga Koowe ambapo serikali imetumia zaidi ya milioni 170.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki usambazaji wa kifusi kwenye bonde la Koowe,Micheweni Pemba.
 Taswira ya mikoko na minazi Koowe,Micheweni Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza maelezo ya ujenzi wa wodi mpya katika hospitali ya wilaya Micheweni kutoka kwa daktari wa wilaya Dk.Rashid Daudi Mkasha .

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la upasuaji la hospitali ya wilaya ya Micheweni Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maabara ya kisasa ya hospitali ya wilaya ya Micheweni Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa mkutano Majenzi,Micheweni Pemba.
 Mbunge wa Viti Maalum Maida Hamad Abdala akihutubia wananchi wa Micheweni ambapo alitoa wito kwa wananchi wa Pemba kuielewa Katiba Mpya na kuona yale ya msingi yalioguswa hasa katika kuwasaidia Wazanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai ali Vuai akihutubia wakazi wa Micheweni
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Micheweni Pemba kwenye viwanja vya Majenzi ambapo aliwaambia wana CCM ,wajiandae ,wajiandikishe  na kuchagua viongozi wazuri.
 Wananchi wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Micheweni Pemba kwenye uwanja wa mikutano Majenzi ambapo aliwaambia viongozi wa vyama vya upinzani wakemee tabia ya baadhi ya wafuasi wao kuwabagua wale wanaohama vyama vyao na kuhamia CCM kwani CCM haijawahi mbagua mtu anayewahama na kuhamia upinzani pia alisisitiza dini haziruhusu mambo ya kubaguana.
Katibu Mkuu wa CCM yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama ambapo aliwasihi wanasiasa kuendesha siasa za vyama vingi kistaarabu ,na kushindana kwa hoja.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.