Tuesday, January 27, 2015

KINANA ATOA DARASA WETE PEMBA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Jimbo la Wete Pemba ambapo aliwataka wananchi hao kusoma vizuri na kuipima Katiba iliyopendekezwa,Katibu Mkuu wa CCM yupo kwenye ziara ya siku 5 ya kujenga na kuimarisha chama Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Wete ,Pemba katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mtemani Wete
 Wananchi kisikiliza kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Nyuso za wananchi zikionyesha kuelewa sana hotuba ya Kinana ambayo imefafanua masuala mengi yakiwemo ya Katiba mpya.
 Mamia ya wananchi wa Wete wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo Pemba kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha Chama.
 Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Abood akihutubia wananchi hao ambao aliwasihi kushiriki chaguzi katika hali ya amani na utulivu.
 Balozi Ali Karume akihutubia wananchi Wete ambapo aliwaambia wananchi hao kufikiria mambo muhimu na ya msingi wao wenyewe badala ya kusubiri kufikiliwa na mtu mwingine.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa jimbo la Ole mara baada ya kupokea taarifa ya Kikundi cha Taifa cha Kampeni Kanda ya Pemba kikundi cha Taarab Maendeleo Kangagani.
 Dk.Maua Daftari akialimia wananchi wa tawi la Kangagani,jimbo la Ole Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wanachuo wa chuo cha ualimu cha Benjamini William Mkapa ambapo alishiriki kazi za ujenzi wa ofisi ya serikali ya wanafunzi,Kojani Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (wa pili kushoto) akishiriki uzikaji wa mabomba ya maji safi na salama jimbo la Mtambwe Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi za kufunga transfoma ,jimbo la Mtambwe ,mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi jiko la mkaa mara baada ya kuwatembelea vijana jimbo la Gando.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kutengeneza malighafi kwa ajili ya kupikia zinazotunza mazingira,Katibu Mkuu wa CCM alitembelea jumuiya ya kutunza mazingira na ufugaji samaki,Gando.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitembelea bwawa la ufugaji samaki lililo chini ya jumuiya ya kutunza mazingira na ufugaji samaki ,Gando.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akila haluwa ya kitutia njia panda ya msiki wa ijumaa,Wete Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya ya Wete kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya.


Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.