Thursday, January 29, 2015

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE PEMBA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mpira Mjimbini,wilaya ya Mkoani,Pemba ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa huu ni wakati wa kupima hoja za msingi,kuisoma na kuielewa Katiba iliyopendekezwa na kuwataka viongozi wa CCM kuchagua viongozi wanaokubalika .
 Wazee wa wilaya ya mkoani wakifuatilia kwa makini.
 Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Mkoani Pemba na kuwataka wananchi hao wajenge utamaduni wa kuwauliza maswali ya msingi yanayohusu maendeleo yao kwa viongozi wao wanapokuja kufanya mikutano.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara na kuwaambia ziara ya Katibu Mkuu wa CCM imeleta mafanikio makubwa Zanzibar kwani wananchi wengi wamekuwa waelewa na kuna kila dalili za kushinda uchaguzi wa 2015 kwa kishindo.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Hadija Abood akiwasisitiza wananchi wa wilaya ya Mkoani kuipigia kura ya ndio Katiba pendekezwa kwani imegusa maslahi ya wananchi wa Zanzibar kwa mapana.
Mwakilishi wa Kuteuliwa na Waziri wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,Vijana na Wanawake Bi.Zainab Omar Mohammed akihutubia wananchi waliohudhuria mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana na kuwataka wananchi hao hasa wanawake kuisoma kwa makini Katiba mpya iliyopendekezwa 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia vijana wa CCM ambao wanahudhuria darasa la Itikadi na Ujasiriamali Chokocho,Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda mgomba kwenye shamba la ushirika wa vijana Utandawazi ambapo vijana zaidi ya 25 wanajishughulisha na kilimo cha migomba Chokocho Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa tawi la CCM Milimuni wilaya ya Mkoani Kusini Pemba,ambapo aliwataka wana CCM kufanya matawi hayo kuwa sehemu za kufanya shughuli za kiuchumi .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua shamba la mboga mboga la kikundi cha Wambaa,wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo  juu ya kilimo cha umwagiliaji kwa matone kutoka kwa Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo na Maliasili Ndugu Suleiman Sheikh Mohamed , Katibu Mkuu alitembelea kikundi cha Wambaa kilichopo wilaya ya Mkoani,Kusini Pemba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Balozi wa shina namba 1, ndugu Ame Vuai Shein wakati akimtambulisha kwa Balozi wa zamani MzeeMakame Bakari Haji (kushoto).
Katibu Mkuu alimtembelea Balozi wa shina namba 1 wa Karadani Chokocho ambapo aliwataka viongozi wa CCM kuiga mfano wa mabalozi kwa kufanya kazi kwa kujitolea.
 Katibu Mkuu wa CCM akishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya skuli ya msingi Tumbi - Chumbaageni,wilaya ya Mkoani, Kusini Pemba.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.