Thursday, January 22, 2015

KINANA AANZA ZIARA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa halmashauri kuu ya mkoa na wilaya ya Kaskazini Unguja ambapo aliwaambia amejifunza kuwa CCM Zanzibar ipo imara sana .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajumbe wa halmashauri kuu za mkoa na wilaya ya Kaskazini Unguja ambapo aliwaambia moja ya dhambi kubwa kwa kiongozi wa CCM ni kubeba mgombea na kumnadi nje ya utaratibu, Katibu Mkuu wa CCM yupo kwenye ziara ya Kuimarisha Chama pamoja na Kuhimiza,kusukuma na kukagua utekelezaji wa Ilani.
 Mwanasiasa mkongwe nchini Ali Ameir ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mbunge wa Jimbo la Donge na Naibu Katibu Mkuu CCM (Zanzibar) akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa kikao cha halmashauri kuu ya mkoa pamoja na wilaya Kaskazini Unguja.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Ali Ameir aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mbunge wa Jimbo la Donge na Naibu Katibu Mkuu CCM (Zanzibar) katikati ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Naibi Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) akipanda mgomba kwenye shamba la akina mama wa Kinyasini wenye umoja unaotambulika kama Tuwe Imara .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda mgomba kwenye shamaba la kikundi cha Tuwe Imara kinachojishughulisha na kulima kilimo cha migomba pamoja na mboga mboga, Bandamaji ,Kaskazini Unguja.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia shamaba la minanasi la kikundi cha akina mama cha Tuwe Imara kilichopo Bandamaji, wadi ya Kinyasini mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Masingini baada ya kushiriki ujenzi wa tawi ambapo aliwashauri wananchi hao wayageuze matawi kuwa sehemu ya kufanya shuguli za kiuchumi na kusaidia kuongeza kipato kwenye matawi hayo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchonga barabara na wananchi kwa Kijijini Kwa Shauri Pili, Barabara hiyo inatoka Shauri pili mpaka Kilwa.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchonga barabara na wananchi kwa Kijini Kwa Shauri Pili, Barabara hiyo inatoka Shauri pili mpaka Kilwa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa nyumba ya madaktari sheia ya Kijini
 Vijana wakionyesha uwezo wa kucheza mchezo wa Judo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea sheia ya Kijini
 Vijana wakionyesha uwezo wa kucheza mchezo wa Judo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea sheia ya Kijini
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Uzio wa kiwanja cha mpira Tazari, Kaskazini Unguja , wengine wanaoshiriki ujenzi na Katibu Mkuu wa CCM ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Ndugu Haji Juma Haji na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar)
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisiliza hotuba ya Saccos ya Vijana Kigunda kabla ya kushiriki ujenzi wa ofisi hiyo.
 Balozi Hamis Makame Faki wa shina namba 3 Nungwi akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kukiri eneo hio lilienda kwa wapinzani kimakosa na kuahidi makosa hayatorudiwa tena.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza alipotembelea shina namba 3 Nungwi  kwa Balozi Hamis Makame Faki.
 Vijana wakihamasisha wakati wa mkutano wa CCM Nungwi

 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini Ali Makame akitoa salaam za ufunguzi wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye vya Skuli ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Wananchi wakifurahia mkutano wa Kinana.
 Mbunge wa Viti Maluum Kidawa Hamisi akitoa hotuba na elimu kwa waliohudhuria mkutano kwenye viwanja vya Skuli, Nungwi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nungwi wilaya ya Kaskazini A kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja
 Wananchi wa Nungwi wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alipokuwa akihutubia ambapo alisisitiza wananchi hao kushikamana kwenye maswala muhimu ya kimaendeleo na kuwapuuza wanaotaka kukwamisha maendeleo.
 Bango la kumkaribisha Kinana Nungwi likiwa na ujumbe wa kumpa hongera kwa kusimamia vyema ilani ya Chama.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai akihutubia wakazi wa Nungwi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakihutubia wananchi wa Nungwi wilaya Kaskazini A ambapo aliwaambia viongozi wa CCM kutenda haki kwani ndio wataheshimika kwa wananchi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Nungwi na kutoa pongezi kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha utiaji saini wa makubaliano ya kuungana kwa chama cha SPLM kutoka Sudani Kusini yaliyofanyika Arusha tarehe 21 Januari na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi mbali mbali.
 Wanachama wapya wa CCM Nungwi wakionesha kadi zao wakati wa kuapishwa.

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.