Wednesday, December 31, 2014

WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI BADO NI TATIZO MKOANI MBEYA


Na Emanuel Madafa,Mbeya,

Jumla ya  1486 wa masomo ya sayansi na hisabati kati ya 2614 wanahitajika mkoani Mbeya i kukidhi mahitaji ya shule zote za sekondari za serikali zilizomo ndani ya Mkoa wa Mbeya.

Akizungumzai changamoto  hiyo  , Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja, amesema idadi hiyo inatokana na takwimu za mwaka 2013.

Amesema, uhitaji wa walimu kwa Mkoa wa Mbeya ni 2614 lakini waliopo ni 1128 pungufu ni walimu 1486 sawa na asilimia 57.

Amesema, kwa upande wa halmashauri mbili likiwemo Jiji la Mbeya na Mbeya vijijini jumla ya walimu 342 wa masomo hayo wanahitajika.

Amesema kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya pekee , inawalimu  237 upungufu ni walimu 255 na wanaohitajika ni 1996 huku halmashauri ya Mbeya inauhitaji wa walimu 751 waliopo ni 129 upungufu ni walimu 77,”alisema.

Amesema, serikali imekuwa ikijitahidi  kuzalisha idadi kubwa ya walimu wa masomo hayo lakini bado changamoto hiyo ni kubwa na hali hiyo inachangiwa na  wanafunzi kuyakimbia masomo hayo pamoja na ukosefu wa vyuo vya ualimu.

Amesema, jambo muhimu linalopaswa kutekelezwa na  wazazi au walezi wa watoto ni kuwahamasisha vijana kupenda kusoma masomo ya sayansi kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza tatizo hili la uhaba wa
 walimu.

Halmashauri ya Busokelo inaupungufu wa walimu wa sayansi na hisabati kwa asilimia 65,Chunya asilimia 42,Ileje asilimia 63, Kyela asilimia 68, Mbarali asilimia 67, Jiji asilimia 56, Mbeya vijijini asilimia 45, Mbozi asilimia 75, Momba asilimia 65 na Rungwe asilimia 30.

Mwisho.
JAMIIMOJABLOG

Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.