Saturday, December 13, 2014

WAGOMBEA CHADEMA WATIMKIA CCM

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu akionyesha kadi nne ya mgombea uenyekiti wa Kitongoji, mgombea uenyekiti wa Kijiji sambamba na Wajumbe wawili kupitia tiketi ya Chadema waliojitoa kugombea na kuhamia CCM
Mtaturu akicheza na vijana wakati wa kufunga kampeni Kijijini Mtwango
 Mgombea pekee mwanamke nafasi ya uenyekiti wa Kijiji cha Ifupila, Kata ya Ifwagi Sevelima Ngunda akiomba kura wakati wa kufunga kampeni

Na Mathias Canal, Mufindi
Wakati ikiwa imebaki siku moja kabla ya kupiga kura kwa ajili ya kuwachagua viongozi watakaowakilisha mitaa, Vitongoji pamoja na vijiji wagombea nafasi ya Uenyekiti wa Kijiji,Kitongoji na wajumbe wawili kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao ni Mgombea uenyekiti wa Kitongoji cha Mpanga Yustin Kadege, Mgombea Uenyekiti wa Kijiji cha Mpanga, Yudita Mutung'e sambamba na wajumbe Anjela Ngenzi na Betson Nkongwa, wametimukia CCM hivyo kuongeza idadi ya mitaa, Vitongoji na Vijiji ambavyo CCM imepita bila kupingwa.
Akipokea kadi hizo kutoka kwa wagombea hao wakati wa mkutano wa kufunga kampeni Wilayani Mufindi, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kutovaa sare za chama siku ya kupiga kura Jumapili ya Disemba 14 mwaka huu.
Mtaturu alisema kuwa watanzania watapiga kura mwa wagombea nafasi ya uenyekiti wa Vitongoji 64,000 Tanzania nzima ambapo pia kuna jumla ya Vijiji 13,000 wakati Mitaa ipo 3000 Tanzania nzima.
Akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Ifupila Kata ya Ifwagi, lakini pia Kijiji cha Mtwango Kata ya Mtwango Mtaturu, alisema kuwa hakuna mwananchi atalayerusiwa kufanya kampeni siku ya chaguzi kwani tayari kampeni hizo zimefungwa Wilayani humo na Tanzania kwa ujumla.
Aidha alitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa familia ya mgombea nafasi ya Kitongoji cha Fukalendi aliyefariki dunia hivi karibuni na kusema kuwa kutokana na msiba huo hakutakuwa na uchaguzi badala yake utafanyika uchaguzi mdogo mara baada ya uchaguzi wa kesho kupita.
"Vyama vya upinzani vimelewa amani na utulivu tulioachiwa na baba wa Taifa hili Mwl Julius K. Nyerere hivyo vinatumia vibaya amani hii kwa kuhamasisha maandamano hatimaye kusababisha wanachi kuuwawa kwa kasi pasipo sababu ya msingi" Alisema Mtaturu
Hata hivyo akiwa Kijiji cha Ifupila Kata ya Ifwagi, Mtaturu alimpongeza Sevelina Ngunda ambaye ni mwanamke pekee anayegombea nafasi ya uenyekiti katika Kata hiyo na Wilaya nzima ya Mufindi.
Mtaturu alisema kuwa mtaji wa CCM sio maneno pekee au kujaza watu kwenye mikutano bali mtaji pekee ni kuwa na watu wenye imani ya kukupigia kura kama ilivyo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo kina wanachama wengi jambo ambalo linasababisha CCM kutamba kushinda kwa kishindo uchaguzi huo.
"Naamini kila mtu anajua kuwa CCM haiombi kura pekee bali inatoa pia elimu juu ya umuhimu wa kupiga kura, hivyo mnapaswa kutambua kuwa kila baada ya miaka 5 uchaguzi wa serikali za Mitaa hufanyika kwa kuwa ndio msingi wa maisha ya wananchi katika maendeleo yao" Alisema Mtaturu
Aidha kesho ni siku iliyokuwa inasubiriwa na watanzania wengi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa ajili ya kuwapata wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji ikiwa ni pamoja na wajumbe ambalo hata hivyo Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho chenye nafasi kubwa ya kuibuka na Mitaa, Vitongoji, na Vijiji kutokana na mtaji iliyonayo ya kupita bila kupingwa kwa asilimia 85% mpaka hivi sasa.

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.