LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 18, 2014

TIBAIJUKA AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari kwenye hotel ya Hyatt Regency Dar Es Salaam, The Kilimanjaro  
.
Dar es Salaam,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Profesa Anna Tibaijuka,amekutana na waandishi wa habari na kuzungumzia sakata la Akaunti ya Escrow,huku akisema haoni sababu ya yeye kujiuzulu kutokana na kudaiwa kuhusika katika sakata hilo.

 Alisema hawezi kufikia uamuzi wa kujiuzulu kwa kuwa hana kosa kwani hajatajwa mahala popote katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG ),ingawa hakupewa nafasi ya kujitetea na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Alisisitiza fedha alizopewa na Rugemalila ni mchango wa Shule ambapo alisema lengo lake kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu bora.
 Alipoulizwa kuhusu kujiuzulu  alisema hawezi jiuzulu kwani haoni sababu ya yeye kujiuzulu.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages