LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 31, 2014

MKUU WA WILAYA YA MBEYA PROFESA NORMAN SIGALLA ATUNUKIWA CHETI CHA UTUMISHI BORA NA MADHEHEBU YA DINI


 Na EmanuelMadafa,
Katika kutambua mchango unaolewa na viongozi wa serikali ndani ya jamii viiongozi wa madhehebu ya dini Mkoa wa Mbeya, wamemtunuku cheti  bora cha utumishi, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Norman Sigalla baada ya kuridhika na utendaji  kazi wake ulioambatana na uwajibikaji mzuri kwa wananchi.

Akizungumza na akizungumza jijini Mbeya , Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Calvary Tabernacle Church Kael Mwaisumo, alisema  kiongozi huyo anastahili kutunukiwa cheti hicho cha utumishi bora kwa kuweza kukidhi vigezo na sifa za uongozi  uliotukuka ndani ya jamii anayoiongoza.

Amesema, baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kwa kuwanyanyasa wananchi na watendaji wa chini jambo ambalo amelipinga kufanywa na kiongozi huyo ambaye ameonekana kuwa mstali wa mbela katika kutatua migogoro ya kijamii husasani ya kidini.

Aidha, akizungumzia tukio hilo, Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mohamedy Mwansasu, ametumia nafasi hiyo kummwagia sifa kiongozi huyo kwa kuhubiri  suala la uadilifu na uwajibikaji kwa watu anaowaongaza hali iliyosaidia kupatikana kwa amani kwa Mkoa wa Mbeya ambao umekuwa na historia ya kuibuka kwa vurugu za mara kwa mara.

Amesema, viongozi wa serikali  wanapaswa kuwa na sifa za uwajibikaji  huku wakitambua  na kuthamini masuala makubwa ya kiutendaji wanayoyafanya kwenye jamii husika.

Hata hivyo, amesema kuwa endapo viongozi wa serikali watatambua kwamba uongozi ni dhahama, wataweza kupunguza kwa asilimia kubwa manung’uniko yanayotolewa na wananchi.
Mwisho.


Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Profesa Norman Sigalla akizungumza na viongozi hao wa madhehebu ya dini ofisni kwakwe baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo.

Maombi 




Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mohamed Mwansasu akizungumza katika hafla hiyo.Picha na David Nyembe wa Fahari News.



No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages