LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 1, 2014

MKE AKIRI MUMEWE BWANA BALENGA KUUZA NYUMBA KWA MFANYABIASHARA HANS MACHA KUTOKANA NA MFANYABIASHARA HUYO KUMDAI MAMILIONI YA FEDHA

DAR ES SALAAM, Tanzania
MKE wa mlalamikaji katika kesi ya kughushi dhidi ya Mfanyabiashara Hans Macha (pichani), amedai mahakamani kwamba mumewe anadaiwa fedha nyingi na mshtakiwa, alishindwa kulipa akaamua kumuuzia nyumba.

Mke huyo Nurya Ahmad (34),ambaye ni shahidi wa upande wa utetezi, amedai hayo leo Desemba Mosi, katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu,Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, kwa kuongozwa na wakili wa utetezi, Deo Ringia.

Nurya amedai mahakamani hapo kwamba nyumba iliyokuwa ya Balenga iliyopo eneo la Kigogo, Dar es Salaam, iliuzwa kihalali kwa Macha baada ya mumewe (Balenga), kushindwa kulipa deni.

“Nafahamu kwamba mume wangu (Balenga), alikuwa andaiwa na Macha, aliniambia mwenyewe kwamba ni fedha nyingi sana, deni halikuwahi kulipwa hatimaye akaniambia kuwa ameeamua kumuuizia nyumba.

“Alikuwa akikopa kwa kuweka rehani hati za nyumba, madeni mengine yalikuwa yakilipwa, tulikuwa katika ndoa kuanzia mwaka 2001 hadi 2012, sijawahi kuona mume wangu akiwa kichaa,” alidai Nurya baada ya kuulizwa kama aliwahi kuona mumewe akiwa kichaa.

Shahidi huyo alihoji mahakamani kwamba hati za nyumba halisi zilifikaje kwa Hans Macha, kama Balenga hakuzipeleka mwenyewe kwake, aliongeza kwamba hajawahi kumsikia mumewe akilalamika
kudhulumiwa nyumba na Macha.

Mfanyabiashara Hans Macha akijitetea alidai  kwamba Ramadhani Balenga alishindwa kumlipa deni la Sh. milioni 879 akamuuzia nyumba iyo ya Kigogo.

Alidai Balengo alikuwa akimtegemea kwa kukopa fedha mara kwa mara kwa ajili ya kuingiza makontena ya vifaa vya umeme au elektroniki.

“Aliletwa na wafanyabiashara wenzangu kwa ajili ya kukopa, nilimpa masharti ya kukopa, aliweka dhamana hati ya nyumba yake ya Mabibo, Manzese, Kigogo, Mbezi Beach, mara ya mwisho Balenga nilikuwa namdai jumla ya Sh. milioni 879, wakati huo nilikuwa na hati zake za nyumba nne.

“Balenga alishindwa kulipa akidai kwamba kontena zake zilikamatwa na kufilisiwa na TRA, aliamua kuniuzia nyumba ya Kigogo, Manzese na nimuongezee Sh. milioni 20 ili tumalizane deni lote.

“Nilipofanya hivyo mbele ya wakili nilikuwa nimempa jumla ya Sh. ilioni 899, nilipomkabidhi fedha ya nyongeza Sh. milioni 20 alinikabidhi hati, siku nyingine tulisaini hati ya kuhamisha umiliki,

Balenga alinikabidhi nyaraka zingine ikiwemo michoro, mikataba ya ujenzi, kibali cha ujenzi, miakataba halisi waliyoingia na kampuni ya ujenzi pamoja na risiti mbalimbali,” Macha alidai.

“Si kweli kwamba nilighushi, Balengo aliniuzia nyumba baada ya kushindwa kulipa deni, naiomba mahakama iyatupe mashtaka yaliyofunguliwa dhidi yangu,”alidai Macha.

Shahidi wa tatu, Mohammed Waziri Mohammed ambaye ni mfanyakazi wa Balenga pia alidai mahakamani kwamba mlalamikaji katika kesi hiyo alikuwa akidaiwa na Macha.

Waziri alidai mara kadhaa alikuwa akienda na mlalamikaji kwa Macha kwa ajili ya kukopa fedha. Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho Jumanne, Desemba 2, 2014

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages