LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 8, 2014

BODI YA UTALII TANZANIA ( TTB ) NA TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA SUNDERLAND (SAFC) ZATANGAZA UTALII WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA


Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kallaghe na Garry Hutchinson Mkurugenzi wa Biashara wa timu ya mpira ya Sunderland wakionyesha jezi ya iliyoandikwa Tanzania yenye rangi za timu hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa matangazo ya Utalii wa Tanzania yanayotangazwa katika uwanja wa timu hiyo kutoka kulia ni Meneja wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bw. Geofrey Meena, Teddy Mapunda mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya (TTB) na kutoka kushoto ni Mdau wa Utalii Bw. Nestor Mapunda na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi.
 3 
Wachezaji wa timu ya Sunderland wakipasha mwili huku wakiwa wamevalia fulana nyeusi zenye maandishi yanayotangaza na kukaribisha watalii na kutangaza utalii nchini Tanzania. 5Matangazo yakiendelea kuonyeshwa kwenye mbao za matangazo wakati mchezo kati ya Chealsea na Sunderland ukiendelea. 6 
Fulana zinazotangazo utalii wa Tanzania ikiwa zimewekwa kwenye vyumba vya kubadilishia jezi wachezaji wa timu ya Sunderland. 7 
Majarida yanayotangaza utalii wa Tanzania yakiwa yamesambazwa kwenye meza katika mgahawa wa timu ya Sunderland kwenye uwanja wao wa Sunderland 8 
Mabango na yanayotangaza utalii wa Tanzania yakiwa yamewekwa kwenye makumbusho ya timu hiyo. 9 
Haya ni baadhi ya mabango yanayoonyeshwa katika uwanja huo wakati wa michezo ya Ligi kuu. 10 
Bendera yenye maandishi ya kukaribisha watalii kutembelea Tanzania ikiwa imepandishwa katika miliongoti katika lango kuu la uwanja huo.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages