LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 25, 2014

RAIS OBAMA AMTUMIA SALAMU ZA KHERI RAIS KIKWETE


 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula akiwasilisha
kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete salamu za kumtakia kheri na afya
njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama leo  jijini Baltimore,
Maryland, Marekani.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  baadhi ya wafanyakazi wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington D.C. wakati
walipomtembelea mjini Baltimore Maryland ambapo balozi Liberata
Mulamula aliwasilisha kwa Rais Kikwete Salamu maalum za kumtakia kheri
na afya njema kutoka kwa Rais Barack Obama leo jijini Baltimore,
Maryland, Marekani.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi
Liberata Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani baada ya kupokea  salamu maalumu za kumtakia
kheri na afya njema  kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo
jijini Baltimore,  Maryland, Marekani.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi Liberata
Mulamula na ujumbe wake wa maafisa waandamizi wa ubalozi  wa Tanzania
nchini Marekani baada ya kupokea  salamu maalumu za kumtakia kheri na
afya njema  kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani leo jijini
Baltimore,  Maryland, Marekani. Picha na Freddy Maro

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages