Thursday, November 20, 2014

MWANDISHI WA HABARI KARASHANI KUZIKWA KESHO SINZA, DAR ES SALAAM

Habari wadau, naomba kuwajulisha kuwa mazishi ya aliyekuwa mwanachama mwenzetu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Baraka Karashani, aliyefariki jana, yatafanyika kesho alasiri katika makaburi ya Sinza, Dar es Salaam. Tunaomba tushirikiane katika kuhifadhi mwili wa mpendwa wetu, ambapo sekreterieti ya TASWA imemteua Majuto Omary ambaye ni Mwenyekiti wa TASWA FC,  Mwani Nyangassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Zena Chande Mhazini Msaidizi  kusimamia michango mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari za michezo nchini kwa ajili ya msiba huo.
Nawasilisha,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
20/11/2014
Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.