Friday, November 14, 2014

KINANA KUANZA ZIARA MKOANI LINDI NA MTWARA NOVEMBA 15


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti,CCM Ofisi ndogo Lumumba.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana anatarajia kufanya ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti,Lumumba jijini Dar es salaam Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye alisema kuwa Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za Sekretarieti ya Halmashauri Kuu Taifa katika mikoa mbali mbali nchini kwa ajili ya kujenga na kuhimiza uhai wa chama na kukagua utekelezazaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 - 2015.

Ziara hiyo itakuwa ya siku 16 na itaanza Novemba 15,2015 ,Katibu Mkuu ataambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye.

Ziara hiyo ya Katibu Mkuu itamwezesha kutembelea  na kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara  katika majimbo yote ya mikoa ya Lindi na Mtwara  ikiwa pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 - 2015, kukutana na wananchi, kuwasikiliza na kwa kushirikiana nao kutafuta majibu ya changamoto zinazowakabili.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.