Thursday, November 27, 2014

KINANA AZOA WAPINZANI NEWALA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Newala Kepteni Goerge Mkuchika wakati wa mapokezi wilayani Newala.
 Wafanyakazi wakibangua korosho kwenye kiwanda cha Micronix Newala ambacho kilitembelewa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kujenga na kuimarisha chama mkoani Mtwara
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuchagua korosho na kuzitenga kutokana na ubora wa madaraja kwenye kiwanda cha Micronix kilichopo Newala mkoani Mtwara.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia)akishiriki kusuka nondo pamoja na mbunge wa Jimbo la Newala Kepteni George Mkuchika kwenye ujenzi wa tenk la maji Kilidu wilayani Newala mkoa wa Mtwara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua kituo cha afya cha Mkwedu wilayani Newala ikiwa sehemu ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
 Jengo la Kituo cha Afya Mkwedu wilaya ya Newala
 Mbunge wa Jimbo la Newala Kepteni George Mkuchika akihutubia wananchi wa Mkwedu mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM kutembelea jengo la kituo cha afya cha Mkwedu wilayani Newala
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwaonyesha wananchi wa Mkwedu kadi ya CUF iliyorejeshwa kwake na Hakika Ibrahim ambaye alirudisha kadi hiyo baada ya kuona na kuelewa utekelezaji wa ahadi za CCM unavyokwenda vizuri.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionnyesha kadi juu zilizorudi kutoka upinzani ambapo wanachama hao kutoka upinzani wameahidi kushirikiana na CCM kwa ajili ya kuleta maendeleo yaTengulengu wilayani Newala.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Tengulengu baada ya kufungua shina la wakereketwa Tengulengu.
 Kikundi cha Kwaya ya CCM Newala kikitoa burudani kabla ya Viongozi kuhutubia kwenye viwanja vya Mahakama Newala
 Mkuu wa Wilaya ya Newala Ndugu Christopher Magala akiwasalamu wananchi wa Newala mjini wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama ya mwanzo na mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akiwasalimu wakazi wa Newala ambapo aliahidi kushirikiana nao vizuri
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Newala ambapo aliwaambia vyama vingi vya siasa hawajui walifanyalo na wamekuwa wakifanya shughuli za kiharakati zaidi kuliko siasa na kuwataka wananchi wa Newala waendelee kukiunga mkono chama chenye mfumo madhubuti cha CCM.
 Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona  akitangaza rasmi kurejea CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mahakama Newala.
  Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona akivua nguo za Chadema mbele ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye.
 Wananchi wakishangilia kurejea kwa  Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona kwenye mkutano wa hadhara uuliofanyika kwenye viwanja vya Mahakama ya mwanzo Newala
  Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Newala Ndugu  Adam Lawi Nangwanda Sijaona akiwa amekabidhi kadi yake na ya mkewe kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Mbunge wa Jimbo la Newala Kepteni George Mkuchika akihutubia wakazi wa Newala mjini ambapo alielezea maendeleo ya utekelezaji wa ahadi za CCM kwenye jimbo lake na pia alitaka wakaguzi watumwe jimboni kwake kuja kukagua ulaji unaoendelea kiasi cha kuwakandamiza wakulima wa korosho wilayani Newala.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Newala kwenye viwanja vya Mahakama ya Mwanzo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali lazima itafute namna ya kuhakikisha uzalishaji wa korosho wote unafanyika nchini kwa kujenga viwanda vya kutosha vya korosho.
 Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akikadidhi pikipiki kwa vijana wa Newala ,pikipiki hizo ni mradi wa CCM wilaya ya Newala kuwakopesha vijana ziwasaidie kwenye shughuli zao za kila siku zikiwemo za boda boda.

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.