Sunday, November 30, 2014

KINANA AITEKA MTWARA MJINI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mtwara mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kazi ya CCM ni kuisimamia Serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa mkoa wa Mtwara ambapo aliwaambia matatizo yao sugu ya korosho, bandari na kukatika kwa umeme lazima yapatiwe ufumbuzi kwa kutaka Mawaziri wa wizara husika kuja na majibu .


 Wananchi wa Mtwara mjini wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa mgeni rasmi akiwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Umati wa wakazi wa Mtwara wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alipokuwa anahutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Chama Cha Mapinduzi ni chama chenye kufuata Kanuni na Taratibu na wale wote ambao watakiuka utaratibu hawana budi kuachia ngazi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mtwara mjini ambapo aliwaambia wapinzani wengi wamekosa sera za msingi na badala yake wanafanya shughuli za kiharakati  na si siasa.
 Wananchi wa Mtwara wakishangilia kila neno kutoka kwa viongozi wao.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisisitiza kwa wananchi hao kuwa wanaipa kura ya ndio CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Desemba 14 mwaka huu.

 Mbunge wa Mtwara Mjini Ndugu Hasnain Murji akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM ulivyotekelezwa vizuri kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa ambapo pia alieleza changamoto zinazowakabili wananchi wa Mtwara mjini hivyo kumtaka Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kusaidia katika kufanikisha baadhi ya mambo ambayo yameonekana kukwamishwa na viongozi wa juu serikalini.

Wananchi wakizunguka gari ya Katibu Mkuu wa CCM baada ya mkutano kumalizika kwenye viwanja vya Mashujaa leo tarehe 30 Novemba 2014.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya jinsi vifaa vya upimaji vya  kisasa vinavyofanya kazi katika maabara kutoka kwa Kanuda Samuel mratibu wa huduma za uchunguzi hospitali ya rufaa ya Ligula mkoani Mtwara.
 Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mkoani Mtwara wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ukumbi wa Pentekosti ,Mtwara mjini
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu Mtwara .
 Mwalimu Dhahabu Christopher wa shule ya sekondari Kitaya ambaye pia ni Mwakili wa walimu shule za sekondari Manispaa akichangia jambo wakati wa kikao cha walimu na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,kikao hicho kilijumuisha waalim wa shule za msingi na sekondari.Share:

KUCHAGUA LUGHA

IDADI YA WATU AMBAO HUTEMBELEA BLOGU HII

KUMBUKUMBU ZA POSTI ZOTE

JISAJILI UPATE TAARIFA KWA EMAIL

Jisajili ili upate taarifa kwa email

Google+ Followers

Powered by Blogger.