Saturday, November 15, 2014

KINANA AANZA ZIARA MKOA WA LINDI LEO

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribishwa wilaya ya Kilwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa ndugu Abdala Ulega mara baada ya kuwasili Somanga,Jimbo la Kilwa kaskazini ikiwa ndio siku ya kwanza ya ziara ya siku 16 katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Lindi Adelina Gefi mara baada ya kuwasili tayari kwa shughuli za kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2010.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na M-NEC wa Nachingwea Fadhil Liwaka.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama na ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Bernard Membe pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakisalimiana na viongozi mbali mbali wa CCM mkoa wa Lindi wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa Skafu wakati wa mapokezi yaliyofanyika Somanga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliofika kumpokea kwa wingi.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana an wananchi waliokuja kumpokea tayari kwa ziara ya Jimbo la Kilwa Kaskazini.

 Msanii wa sanaa za kucheza na vichekesho Ally Said Abubakary akionyesha mbwembwe  zake wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozan na viongozi wengine kwenda kukagua moja ya miradi iliyopo Somanga.


 Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Ndugu Abdala Ulega akisalimia wananchi wa  kata Somanaga waliojitokeza kushiriki na Katibu Mkuu wa CCM katika ujenzi wa nyumba ya kulala wageni ya kikundi cha Mwamko (VICOBA)
 Mheshimiwa Bernard Membe akisalimiana na wananchi wa kata ya Somanga waliojitokeza kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kushiriki nae ujenzi wa mradi wa nyumba ya kulala wageni ya kikundi cha Mwamko.
Mkuu wa mkoa wa Lindi akisalimia wananchi

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi N\pe Nnauye akitoa salaam kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa akizungumza wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika mkoa huo .
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM baada ya kumvisha mgolole wenye rangi za CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Somanga mara baada ya kushiriki ujenzi  wa mradi wa nyumba ya kulala wageni ya kikundi cha Mwamko (VICOBA)

Katibu Mkuu wa CCM akizungumza na wananchi wa kata ya Somanga ambapo aliwaambia kuwa Chama cha Mapinduzi hakiwezi kuunga mkono uvuvi haramu kwa ajili ya kupata kura.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman akishiriki ujenzi wa mradi ya nyumba ya kulala wageni ya kikundi cha VICOBA Mwamko,Somanga.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.